Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mume achinja mke, ajinyonga

C50d1a00ea05e9bcdec2322f68472c3d Uhalifu

Fri, 17 Jul 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

MKAZI wa Kijiji cha Mipanga Kata ya Majimoto wilayani Mlele mkoani Katavi, Kisabo Joseph (21) anadaiwa kumuua mkewe Dalali Malango (20) kwa kumchinja kwa sababu ya kunyimwa unyumba kwa muda mrefu.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, Benjamin Kuzaga alithibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo alisema, baada ya tukio hilo, Joseph aliutupa mwili wa mkewe jirani na makaburi na yeye akajinyonga.

Inadaiwa mwanaume huyo alichukua uamuzi huo kwa kuwa alikuwa amekasirishwa na vitendo vya mkewe kukataa kufanya nae tendo la ndoa kwa muda mrefu.

“Jioni ya siku ya tukio mume alimvizia mkewe alipokuwa akienda kuchota maji kwenye bwawa ambalo linabubujika maji ya moto...alimvamia mkewe na kumchinja...maofisa wa polisi walipokuwa wakimsaka mtuhumiwa wa mauaji hayo (Kisabo) walikuta mwili wake ukining’inia kwenye kamba iliyofungwa kwenye tawi la mti akiwa amejinyonga jirani na sehemu alipomchinja mkewe ambayo ni jirani na eneo la makaburi,” alisema Kamanda Kuzaga.

Alisema, inasadikika Joseph alimchinja mkewe saa moja usiku Julai 14 mwaka huu katika kijiji cha Mipanga. Alisema, uchunguzi wa awali umebaini kuwa chanzo cha mauaji hayo ni kuwa, kwa muda mrefu dalali alikuwa akikataa kufanya tendo la ndoa na mumewe kwa sababu alizokuwa akizifahamu yeye.

Kwa mujibu wa Kamanda Kuzaga, Joseph alimshuku mkewe kuwa alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanaume mwingine na ndio maana alikuwa akikataa kufanya nae tendo la ndoa.

Ndugu wa Joseph walilieleza gazeti hili kuwa, alfajiri ya Julai 15 mwaka huu, mdogo wa kijana huyo alijihimu kwenda mnadani ndipo alipouona mwili wa kaka yake ukiwa unaning’inia kwenye kamba iliyofungwa kwenye tawi la mti akiwa amejinyonga.

“Juzi kulikuwa na sherehe ya harusi ambapo pia kaka yangu Kisabo alihudhuria, baada ya kusheherekea kwa amani nilienda katika kijiji cha jirani cha Mabambasi na siku iliyofuata saa kumi na mbili jioni nilipigiwa simu kuwa kaka yangu Kisabo amejinyonga. Baada ya muda si mrefu, nikaelezwa kuwa pia mkewe amechinjwa na mwili wake umekutwa ukiwa umetupwa kwenye shimo jirani na eneo la makaburi, “ alisema Ngereja Joseph.

Chanzo: habarileo.co.tz