Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mume aangua kilio mahakamani akielezea jinsi mke wake alivyouawa

65747 MAHAKAMA+PIC

Sat, 6 Jul 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. JohnThomas ambaye ni mume wa marehemu Silivesta Njau ameieleza Mahakama Kuu ya Tanzania jinsi alivyomkuta mke wake akiwa amepigwa kichwani, povu likimtoka na shoka lililotumika kumuua pembeni yake likiwa na damu iliyokuwa imesambaa kuanzia kwenye korido hadi chumba alichokuwa akilala.

Machi 27, 2014 Oliana Shabani anadaiwa kuwa alitenda kosa la kumuua kwa makusudi Silivesta maeneo ya Vingunguti Miembeni, Dar es Salaam nchini Tanzania.

Shahidi huyo jana Ijumaa Julai 5,2019, aliangua kilio wakati akitoa ushahidi wake mbele Hakimu Pamela Mazengo.

Huku akiongozwa na wakili wa Serikali, Grace Mwanga, shahidi huyo alidai  Machi 27,2014 saa 11 , alipigiwa simu na dereva aliyekuwa anamrudisha mtoto wake nyumbani na kudai amegonga geti lakini halifunguliwi.

Thomas alidai alikodi pikipiki hadi nyumbani kwake na kukuta watu wengi ndipo alipotaka kuingia ndani, alikuta geti limefungwa na msichana wa kazi Oliana ambaye ndiye mshtakiwa aliondoka na funguo wa geti, ndipo alipanda ukuta na kumkuta mke wake akiwa kwenye korido hajitambui.

Thomas alidai mke wake alikuwa ameumizwa eneo la kichwani karibu na sikio huku povu likimtoka mdomoni alimchukua na kumuwahisha Hospitali ya Amana lakini wakati anapatiwa matibabu alifariki dunia.

Pia Soma

Alidai waliuchukua mwili na kuupeleka hospitali ya Taifa Muhimbili na baadaye alirudi nyumbani akiongozana na baadhi ya polisi, walipofika nyumbani walikuta shoka jipya likiwa na damu na walipoingia chumbani walikuta kabati limevunjwa.

"Eneo la sebuleni damu zilikuwa zimetapakaa hadi kwenye mkeka, mito na nguo ya marehemu ikiwa imechanwa na tulipoangalia kabatini tuliona limevunjwa huku nguo zikiwa zimetupwa chini na walipopekua walikuta simu aina nokia, saa ya mkononi, dhahabu zote na begi ya mkononi na baadhi ya nguo zilikuwa zimechukuliwa na mshtakiwa Oliana,” alidai Thomas.

Alidai baada ya kumpumzisha mke wake walisafiri pamoja na askari polisi hadi Arusha na kumkuta mshtakiwa akifanya kazi za ndani , walitoa taarifa kwenye uongozi wa mtaa na walipoingia kwenye chumba anacholala kukikagua walikuta vitu vya mke wake marehemu ikiwemo simu ya mkononi aina ya Nokia, funguo za geti, Kamera, begi ya mkononi, mtandio na vitambulisho vya benki.

Chanzo: mwananchi.co.tz