Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mtwara: Mwanamke ajeruhiwa kwa kukatwa mapanga kisa simu ya 24,000/=

Panga 3 Sehemu ya mwili aliyokatwa mapanga Josephine Boniface

Fri, 28 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanamke mmoja Mkazi wa Kijiji cha Lyowa Mkoani Mtwara, Josephine Boniface (30) amejeruhiwa kwa kukatwa na mapanga kwenye miguu yake yote miwili na mumewe baada ya kupoteza simu ndogo (Kiswaswadu) yenye thamani ya Tsh. 24,000.

Josephine anasema wakiwa kwenye sherehe za ngoma za jando na unyago usiku kijijini hapo, Mumewe alimkabidhi simu hiyo ndogo ili amhifadhie lakini baadaye alipokea taarifa ya kushtukiza ya kuunguliwa moto nyumba ya Mdogo wake kijijini jirani na kujikuta anapoteza simu bila kujua "tuliporudi nyumbani, nilimwambia Mume wangu ambaye alipata hasira na kisha kuchukua panga kuanza kunipiga nalo sehemu mbalimbali za mwili na kunijeruhi miguuni"

“Mume wangu alipofika nyumbani hapa kwa Mama, tukampa taarifa za tukio la kuunguuliwa kwa moto nyumba ya Ndugu zetu na Mimi ndio nikamwambia kwamba nimedondosha simu, akasema 'aah haiwezekani kudondosha simu yangu Mimi nataka simu yangu, sijui habari za moto, wala habari za nini, sitaki chochote, nataka simu yangu, akaanza kunipiga" anasema Josephine Hassan.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Lyowa, Mohamed Mmunda amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema Mwanaume huyo ametoroka baada ya tukio.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live