Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mtunza hazina wa kikoba auawa kwa kupigwa jiwe

Mauaji Mlsk Mtunza hazina wa kikoba auawa kwa kupigwa jiwe

Sun, 30 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kijana wa miaka 15 (jina linahifadhiwa), mkazi wa Kijiji cha Ngareni, Kata ya Ngoyoni, wilayani Rombo, anashikiliwa na Jeshi la Polisi akidaiwa kumuua mama yake mdogo, Taudensia Massawe (62) kwa kumpasua kichwa akitumia jiwe wakati akikata majani ya ng'ombe.

Tukio hilo linadaiwa kutokea Aprili 24, mwaka huu baada ya kijana huyo kumwambia marehemu akamwonyeshe sehemu ya kukata majani ya ng'ombe na alipofika eneo aliloonyeshwa alimvizia wakati ameinama akikata majani na akampiga na jiwe lililompasua kichwa.

Kijana huyo anadaiwa kufanya mauaji hayo kwa lengo la kupora fedha za Vicoba ambazo mama huyo alikuwa mweka hazina na alikuwa na sanduku la fedha hizo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live