Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mtumishi wa Seikali auawa baa na mkewe kisa meseji za simu

Mauaji Baa Ke Mtumishi wa Seikali auawa baa na mkewe kisa meseji za simu

Sat, 16 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Charles Okoth Onyango (31) ameuawa baada ya kuchomwa kisu kifuani wakati wakiwa baa kutokana na wivu wa mapenzi.

Jeshi hilo la Polisi katika Kaunti ya Homa Bay nchini Kenya linasema tukio hilo lilijiri wakati wa ugomvi kuhusu simu ambapo mke alitaka kusoma meseji (SMS) za mumewe wakati wakipiga vyombo (pombe).

Kwa mujibu wa jeshi hilo, Onyango alikuwa mtumishi wa Serikali katika Kaunti ya Homa Bay na alikata moto eneo la tukio baada ya kujeruhiwa vibaya kufuani.

Kwa mujibu wa walioshuhudia, Onyango alifika kwenye baa hiyo na kuagiza vinywaji ambavyo alifurahia pekee yake akiwa kwenye kona moja ya baa hiyo.

Baadaye mwanamke aliyetajwa kuwa ni mkewe, alijiunga naye na kuanza kunywa pombe.

Wawili hao walipokuwa wanaendelea kunywa vyao ndipo mzozo ukazuka kati yao. Inadaiwa mke aliomba simu ya mumewe asome meseji ambazo alikuwa akizipokea.

Onyango anaripotiwa kukataa kutoa simu yake na badala yake kuanza mzozo mkubwa na kuvutia masikio ya watu wengine.

Mzozo huo ulipofika kilele chake, mwanamke huyo alichomoa kisu na kumchoma Onyango kifuani.

Alikuwa amebeba kisu hicho kwenye mkoba wake kwa kile kinachooneka kuwa alikuwa amejiandaa kwa tukio hilo.

Kwa mujibu wa Chifu wa Kata ya Homa Bay mjini, Joshua Ochogo, mtuhumiwa alimchoma mwendazake kisu mara moja kabla ya kuanguka na kuaga dunia.

Kamanda wa Polisi wa Kaunti ya Homa Bay, Sammy Koskeyi anasema uchunguzi katika kisa hicho unaendela huku mwili wa marehemu ukipelekwa kuhifadhiwa katika Hospitali ya Mafunzo na Rufaa ya Homa Bay kwa ajili ya mazishi. Mtuhumiwa anashikiliwa na Polisi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live