Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mtumishi baraza la ardhi afikishwa Mahakamani na TAKUKURU

PCdwq3eCB5.png Mtumishi baraza la ardhi afikishwa Mahakamani na TAKUKURU

Thu, 10 Sep 2020 Chanzo: millardayo.com

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Mkoa wa Manyara, imemfikisha Mahakamani Mtumishi wa baraza la ardhi Wilaya ya Babati,  Ruth Reniel Semkuyu kwa makosa ya kudai na kuomba rushwa ya shilingi laki moja.

Akisomewa mashtaka  hayo mbele ya Hakimu  Mkazi wa Mahakama ya Mkoa wa Manyara, Mwendesha Mashtaka wa TAKUKURU Evelyne Onditi ameeleza kuwa,  kesi ya Jinai namba CC.155/2020 imesomwa Septemba 9 mwaka huu mbele ya Hakimu mkazi mfawidhi wa Mahakama hiyo Simon Kobelo.

Mwendesha mashtaka huyo amesema, baada ya kusomewa Mashtaka hayo, mtuhumiwa huyo alikana na kurudishwa rumande baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana.

Onditi amesema kesi hiyo itatajwa tena Mahakamani hapo Septemba 23,2020.

‘KIPUA’ STAA ANAEHESHIMIKA KWAO, AMEFANYA TAMASHA IKULU, MREMBO ANAEMMILIKI, ANAJAZA UMATI

Chanzo: millardayo.com