Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mtuhumiwa wa mauaji ya mke,mtoto afikishwa kortini

Mtuhumiwa Mds Mtuhumiwa wa mauaji ya mke,mtoto afikishwa kortini

Fri, 3 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mtuhumiwa August Matemu, amefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi, akikabiliwa na mashtaka mawili ya mauaji ya mke wake na mtoto.

Mtuhumiwa wa mauaji ya mke wake na mtoto, August Matemu (katikati), akiwa chini ya ulinzi wa askari polisi huku akishikiliwa na baba yake mzazi, John Bosco (kulia) na baba mkubwa, Finuel Patro (kushoto), baada ya kufikishwa kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi mkoani Kilimanjaro jana.

Akisoma mashtaka hayo jana mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama hiyo, Jenipher Edward, Wakili wa Serikali, Kassimu Nasir, alidai kuwa Februari 22, mwaka huu, Kijiji cha Mamba Mero, Kirua Vunjo, mshtakiwa anadaiwa kumuua kwa kukusudia mke wake, Fausta Tesha akiwa amelala kwenye nyumba waliyokuwa wakiishi.

Wakili Nasri alidai katika kosa la pili, siku hiyo hiyo, August anadaiwa kutekeleza tukio lingine la mauaji kwa makusudi kwa mtoto, Rodrigo Mgaya. Kwa mujibu wa Wakili Nasri, upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika.

Hakimu Mkazi, Jeniffer alisema kesi hiyo haina dhamana huku akimtaka mshtakiwa kutojibu chochote mbele ya mahakama hiyo kwa kuwa, haina uwezo wa kusikiliza kesi hiyo. Kesi hiyo imeahirishwa hadi Machi 22, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live