Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mtuhumiwa kesi ya teleza ayakana maelezo adai alilazimishwa kusaini

Thu, 3 Oct 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Kigoma. Mshtakiwa Hussein Rajabu (28), anayetuhumiwa kwa kosa la kuvunja nyumba na kujeruhiwa nyakati za usiku kata ya Mwanga wilayani hapa mkoani Kigoma, amekana maelezo ya onyo aliyochukuliwa katika kituo cha polisi na kudai si yake isipokuwa alilazimishwa kusaini.

Akizungumza leo Jumatano Oktoba 2, 2019 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kigoma, mtuhumiwa huyo baada ya shahidi wa tano ambaye ni wa mwisho kutoa ushahidi wake, askari wa kitengo cha upelelezi wa makosa ya jinai Tanzania, Elias Ndege kwa upande wa mashtaka, amesema maelezo hayo si yake.

Mshtakiwa huyu mbali na kukana maelezo hayo ya onyo aliyoandikishwa wakati amekamatwa akiwa kituo cha polisi kati Kigoma, amemuomba Hakimu Mkazi anayesikiliza kesi hiyo kutopokea kielelezo hicho kama ushahidi katika kesi hiyo.

“Mimi nilikamatwa nikiwa wilayani Kasulu ambako ndiyo ninaishi na nilipokamatwa nilipelekwa moja kwa moja polisi na kuwekwa ndani bila kuambiwa kosa langu, sikuwahi kuhojiwa na mtu yeyote na siku iliyofuata niliambiwa nisaini maelezo yaliyokuwepo kwenye karatasi na nilipojaribu kuhoji niliambiwa sitakiwi kusema chochote ila kusaini tu,” amedai  mtuhumiwa huyo.

Hakimu Mkazi mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Kigoma, Kenneth Mutembei amesema hatua ya mshtakiwa kukataa maelezo aliyochukuliwa wakati amekamatwa akiwa kituo cha polisi, hakuweza kumzuia yeye kutopokea maelezo hayo kama kielelezo katika kesi hiyo.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Oktoba 9, Mwaka huu kwaajili ya kutoa ushindi kwa upande wa utetezi ambapo mshtakiwa alisema katika ushindi huo atajitetea mwenyewe.

Pia Soma

Advertisement
Kesi hiyo namba 57 ya mwaka 2019, inadaiwa mnamo Mei 20, 2019, huko maeneo Mwanga Vamia wilayani hapa mkoani Kigoma, mshatakiwa alitenda makosa mawili likiwamo la kuvunja nyumba usiku kwa nia ya kutenda kosa la kujeruhi na kosa la kubaka.

 

 

Chanzo: mwananchi.co.tz