Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mtuhumiwa kesi ya kunajisi aendelea kusota rumande

Pingu Law Mtuhumiwa kesi ya kunajisi aendelea kusota rumande

Tue, 29 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mshtakiwa wa kesi namba 62 ya mwaka 2023, Elpidius Edward (22) anayetuhumiwa kufanya uhalifu katika Kanisa Kuu la Kiaskofu Jimbo Katoliki la Geita atasalia rumande ushahidi ukiwa haujakamilika.

Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoa wa Geita, Johari Kijuwile ameeleza hayo baada ya kusikiliza ushahidi wa msaidizi ofisi ya Askofu wa Jimbo Katoliki la Geita, Padri Charles Kato.

Hiyo inakuja kufuatia Mtuhumiwa kutotimiza mashariti ya dhamana yanayomtaka kuwa na wadhamini wawili watakaosaini hati ya fedha taslimu ama mali isiyohamishika yenye thamani ya Sh milioni 24.1.

Akitoa ushahidi wake mbele ya Mahakama, Padri Kato amesema alipata taarifa za uhalifu wa Kanisa hilo lililopo mtaa wa Jimboni usiku wa Februari 26, 2023 majira ya saa nane usiku alipoarifiwa kwa simu.

Amesema wakati mtuhumiwa anaingia Kanisani na kufanya uhalifu mlinzi wa Kanisa alikuwa peke yake na hakuwa karibu na jengo la kanisa kutokana na ukubwa wa eneo lake la kazi.

Padri Kato amebainisha hata baada ya mlinzi huyo mmoja kuwasili eneo la Kanisa hakuweza kuingia ndani ya kanisa kumdhibiti muhalifu kwani sheria haimuruhusu kuingia eneo la madhabahu bila ruhusa.

Amesema zuio hilo lilimfanya mlinzi kusubiri ruksa hali iliyotoa nafasi kwa muhalifu kuendelea kufanya uharibifu mkubwa ndani ya kanisa mpaka pale padri Kato alipowasili na walinzi wengine wa kampuni.

Mtuhumiwa wa kesi hiyo, Elpidius alihoji iwapo mlinzi haruhusiwi kuingia ndani ya kanisa je, ni nani aliyemkamata, na kwa nini watoe ushahidi ingali kuna kamera za ulinzi?

Padri Kato alijibu mtuhumiwa alianza kwa kuharibu mfumo wa kamera za ulinzi (CCTV) na ndio maana hakuna picha za mtuhumiwa hazijaletwa mahakamani na alikamatwa baada ya walinzi kuruhusiwa.

Baada ya kusikiliza ushahidi huo, Hakimu Johari ameahirisha kesi hiyo mpaka itakapotajwa tena Septemba 11, 2023 kwa ajili ya kuendelea kusikiliza ushahidi na kuamuru mtuhumiwa kurejeshwa rumande.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live