Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mtuhumiwa aomba kukiri makosa kesi iishe

UI71hnD3.jpeg Mtuhumiwa aomba kukiri makosa kesi iishe

Fri, 1 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mshitakiwa Mussa Salum Mohammed, ameiomba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuendelea na ombi lake la kukiri makosa ili kumaliza kesi.

Upande wa utetezi umeiomba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuendelea na hatua ya kusaini mkataba wa makubaliano ya kuomba kukiri makosa baina ya mshtakiwa na ofisi ya Mkurugenzi ya Mashitaka (DPP).

Hatua hiyo imekuja baada Wakili wa Serikali, Tumaini Maingu, kueleza mahakama hiyo kuwa, mshitakiwa huyo alishawahi kuandika barua ya kuomba kukiri makosa yake katika ofisi ya DPP, lakini hakufikia mwisho kwa kuwasilisha mkataba.

"Tunataka kujua kama mshitakiwa ataendelea na pre bargaining yake au la," amedai Wakili Maingu

Ndipo Wakili wa utetezi, Josephat Mabula, akadai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi, kuwa mshitakiwa huyo aliwahi kuomba kukiri kosa lake la tulifikia makubaliano ya kifungo cha miaka mitatu.

"Kwa hatua ya leo, kwamba mtuhumiwa aulizwe kama ana nia ya kuendelea na pre bargaining yake au la," alidai Mabula.

Hakimu Shaidi alimuuliza mshitakiwa huyo kama atahitaji maridhiano, ndipo alijibu kuwa anahitaji kuendelea na hatua ya kusaini mkataba waliokubaliana na DPP kumaliza kesi hiyo.

Hakimu Shaidi alimaliza shauri hilo kwa kusema kesi itasikilizwa tarehe Septemba 8, 2023 na kuwataka mashahidi waje na ushahidi uliojitosheleza.

Inadaiwa kuwa Juni5 2020 eneo la bandari ya Dar es Salaam mshitakiwa Mohammed alikamatwa na dawa za kulevya aina ya heroin zenye uzito wa gram 101.71.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live