Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mtuhumiwa achezeshea kichapo kisha aogeshwa tope!

Ogatope.png Mtuhumiwa akiogeshwa 'Maji ya Baraka'

Tue, 19 Apr 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kijana ambaye hajafahamika haraka jina lake anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 25 mpaka 30 mkazi wa Igoma halmashauri ya mji wa Njombe amenusurika kifo kutoka kwa wananchi wenye hasira kali katika mtaa wa Mpechi eneo la Lutilage mara baada ya kukamatwa akiwa ameiba vitu mbali mbali Ikiwemo TV,Godoro,Blanketi na Mtungi mdogo wa gesi.

Luo Lameck Mgeni ni mzee aliyekuwa amempangisha awali katika nyumba yake kabla ya kumfukuza kutokana na tabia ya wizi anasema anashangaa kuona kijana huyo ameondoka kwake lakini amerudi na kuiba kwenye moja ya nyumba ya familia yake.

“Leo nikasikia kule nyumbani wameboboa nikauliza wameiba nini,kuingia mle ndani tukaona tandiko halipo na vitu vingine amechana chana ameweka nje”alisema Mzee Mgeni

Awali wananchi wenye hasira kali walimtia nguvuni kijana huyo na kuanza kumchezeshea kichapo cha mbwa koko kisha kumuogesha maji yaliyotuama yenye tope zito.

Hata hivyo kabla kijana huyo kufikiwa na hali mbaya kutokana na kipigo,Jeshi la Polisi lilifika eneo la tukio na kufanikiwa kumuondoa eneo hilo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live