Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mtoto wa wazazi waliojiua apata msaada wa matibabu

53286 Pic+watoto

Sat, 20 Apr 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Tabora. Mtoto Chiku Kudona ambaye wazazi wake walijiua kutokana na kuugua kwake kichwa, hatimaye amepata msaada wa matibabu.

Mtoto huyo sasa atapatiwa matibabu pasipo malipo katika hospitali ya Rufaa ya Bugando iliyopo jijini Mwanza.

Akizungumza leo Jumamosi Aprili 20, 2019, Adam Kalonga ambaye ni babu yake Chiku amesema wamepewa taarifa kuwa wamekuja watu wa Bugando kumchukua mtoto kwa ajili ya matibabu.

"Tunalishukuru sana gazeti la Mwananchi kwa namna lilivyofuatilia suala la mtoto huyu," amesema Kalonga.

Kwa upande wake, mwenyekiti wa kitongoji cha Gombe One, katika kijiji cha Kigombe, Gerson Maganga ameshukuru kwa namna suala la mtoto huyo lilivyopewa kipaumbele.

"Tunalishukuru sana gazeti la Mwananchi na hatuna budi kusema asante, " amesema.

Related Content



Chanzo: mwananchi.co.tz