Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mtoto wa miaka mitatu amuua dada yake kwa risasi

Bastola Mtoto wa miaka mitatu amuua dada yake kwa risasi

Tue, 14 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mtoto mwenye umri wa miaka mitatu amemuua kwa bahati mbaya dada yake (17) kwa kumpiga risasi katika mji wa Houston, Texas nchini Marekani.

Kamanda wa polisi katika eneo hilo, Harris Ed Gonzalez amesema tukio hilo lilitokea licha ya kuwepo kwa watu wazima watano nyumbani hapo wakiwemo wazazi wa watoto hao nyumbani.

“Wanafamilia waliposikia mlio mmoja wa risasi walikimbilia chumbani na kumkuta mtoto huyo akiwa sakafuni,” alisema Gonzalez huku akisisitiza kuwa risasi ilionekana imefyatuliwa bila kukusudiwa.

Kulingana na utafiti uliofanywa na kituo cha cha Pew, takriban asilimia 40 ya makazi ya watu nchini Marekani yana bunduki.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live