Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mtoto wa miaka minne aliyepotea apatikana

Wed, 3 Oct 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mtoto wa miaka minne anayeishi Tabata Mawenzi  Paulo Mgaya ambaye taarifa zake zilisambazwa kwenye mitandao ya kijamii kwamba amepotea, jana amepatikana  akiwa hai.

Akizungumza na Mwananchi leo mzazi wa mtoto huyo Jimson Mgaya amesema  kwamba mtoto wake aliyekuwa amepotea ghafla nyumbani kwao Tabata jioni saa 12 katika mazingira ya kutatanisha alikutwa na wasamaria wema Tabata Chang’ombe saa tatu usiku.

Amesema wasamaria wema walioona ujumbe kwenye mitandao ya kijamii ambapo aliweka picha ya mtoto pamoja na namba za simu walimpigia na kumfahamisha kwamba wamemuona akilia.

“Walinipigia simu wakisema kwamba wamemuona analia na baada ya kumuuliza anatokea wapi  hakuweza kujieleza hivyo wakaamua kumpeleka kwa mjumbe wa eneo hilo.

“Mimi nimefurahi jitihada za majirani na watu wanaosoma mitandao ya kijamii kwa kutoa msaada wa kupatikana mwanangu,’’amesema

Amewataka wazazi kuwa makini na watoto wao kwa sababu hata yeye hajui kitu kilichomkuta mtoto wake huyo,kwamba ni mtu aliyemchukua akamwacha huko (Tabata) au ni mtu wa aina

 

Chanzo: mwananchi.co.tz