Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mtoto wa miaka 9 akamatwa na polisi akiendesha gari

Polisi Trafiki Barabarani Mtoto wa miaka 9 akamatwa na polisi akiendesha gari

Sun, 28 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Maafisa wa Usalama barabarani (trafiki) katika barabara ya Mombasa wamemkamata mtoto mdogo shule mwenye umri wa miaka 9 akiendesha gari.

Katika kisa kilichotokea juzi Jumatano, Agosti 24, mtoto huyo alisemekana kuwa alikuwa akiendesha gari la babake 'Saloon' wakati akielekea shuleni.

Maofisa wa kutekeleza sheria wanaodhibiti trafiki katika barabara ya Mombasa walimwona akiendesha gari huku akiwa amevalia sare za shule kupitia dirisha la mlango.

Babake alikuwa ameketi na yeye mbele huku mtoto wa miaka saba anayeaminika kuwa dada ya mtoto aliyekuwa akiendesha gari akiwa kwenye kiti cha nyuma. Maofisa hao walijaribu kumsimamisha lakini alipuuzilia na kuendesha gari kwa kasi kwa lengo la kuepa polisi.

Maofisa hao walimfuata mtoto huyo wa miaka 9, na gari lao katika barabara kuu kwa takriban kilomita 2 kabla ya gari hilo kuzuiliwa. "Kuruhusu watoto kuendesha gari kunaweka maisha ya madereva wengine hatarini. Pia ni kinyume cha sheria za trafiki nchini," mkuu wa polisi wa Athi River Mary Njoki alisema.

Hata hivyo, babake alikamatwa na kuzuiliwa katika Kituo cha Polisi cha Athi River huku mwanawe na bintiye wakirudishwa shuleni na polisi.

Polisi walisema kuwa baba huyo atafikishwa katika mahakama ya Mavoko kaunti ya Machakos kujibu mashtaka yaliyowekwa na maafisa wa polisi wa trafiki. Leseni yake pia inaweza kufutwa.

Ni lazima mtu afikishe umri wa miaka 18 ili apewe leseni ya kuendesha gari nchini Kenya. Wageni wanatakiwa kuwa na leseni kamili ya kuendesha gari halali katika nchi wanamoishi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live