Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mtoto wa miaka 17 mbaroni kwa kuoa, kumpa ujauzito binti wa miaka 14

Mimba Wanafuzi Mtoto wa miaka 17 mbaroni kwa kuoa, kumpa ujauzito binti wa miaka 14

Fri, 3 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

MTWARA, Tanzania: JESHI la Polisi mkoani Mtwara linakusudia kumfikisha mahakamani kijana mwenye umri wa miaka (17) mkazi wa Kijiji cha Mtunguru wilayani Newala, kwa tuhuma za kumuoa na kumpa ujauzito mwanafunzi wa darasa la sita (14).

Akitoa taarifa hiyo wiki hii alipozungumza na HabariLEO, Ofisa Ustawi wa Jamii wilayani humo, Bakari Mnali alisema kitengo hicho kilifanya jitihada ya kumhoji msichana huyo na kumpima magonjwa mbalimbali na kugundulika kuwa ana ujauzito wa zaidi ya miezi mitatu.

Alisema mwanafunzi huyo alikuwa akisoma katika Shule ya Msingi Mtunguru wilayani humo na aliacha shule tangu Oktoba, mwaka jana akidai kuwa wazazi wake wameshindwa kumhudumia mahitaji yake ya shule. Msichana huyo ni mkazi wa kijiji hicho cha Mtunguru wilayani humo na inadaiwa baba yake mzazi aliacha kumpatia mahitaji hayo ya shule tangu akiwa darasa la awali shuleni hapo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live