Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mtoto wa miaka 10 mbaroni kwa kumuua aliyekuwa akigombana na mama yake

Isaac And Rodgers 800x450 Mbaroni kwa kumuua adui wa mama yake

Wed, 8 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 10 kutokea jimbo la Florida nchini Marekani amekamatwa na kushtakiwa kwa kosa la mauaji ya Mwanamke aliyehusika katika ugomvi na mama yake.

Idara ya Polisi ya Orlando ilimchukua Mtoto huyo na kumuweka chini ya ulinzi kwa tuhuma za mauaji ya daraja la pili na kumpeleka kwenye kituo cha Watoto watukutu.

Mauaji ya Lashun Rodgers (41) (pichani kulia) anayeonekana kwenye picha kushoto yalitokea Mei 30, 2022 wakati akigombana na mama wa mtoto huyo, Lakrisha Isaac (31) anayeonekana kushoto.

Polisi wameeleza kuwa, mpenzi wa Lashuin alijaribu kusuluhisha ugomvi huo lakini haikuwezekana.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, wakati ugomvi ukiendelea, Isaac alimpa mtoto wake amshikie begi ambalo kumbe ndani yake kulikuwa na bastola, mtoto huyo alichukua bunduki ya mama yake na kufyatua risasi mbili ambapo moja ilimopata Lakrisha kichwani, alikimbizwa hospitali lakini alifariki.

Mama wa mtoto huyo alikamatwa muda mfupi baada ya tukio na anakabiliwa na mashtaka kadhaa ikiwemo kuua bila kukusudia, shambulio la kikatili kwa kutumia bunduki na kutelekeza mtoto.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live