Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mtoto wa mganga afariki kwa kunywa dawa ya kusafishia nyota

Habarileo Tz 140672535 314317663324008 5381641829105179064 N 640x400 Mtoto wa mganga afariki kwa kunywa dawa ya kusafishia nyota

Wed, 20 Jan 2021 Chanzo: millardayo.com

Mtoto Juma Megejuwa mwenye miaka 12 mkazi wa Kijiji cha Mwaningi katika Kata ya Bulige wilayani Kahama mkoani Shinyanga, amefariki dunia baada ya kunywa dawa ya kienyeji kwa mzazi wake ambaye ni mganga wa kienyeji kwa lengo la kusafishwa nyota.

Aidha, watu wawili ambao ni ndugu, Loya Ngusa (66) na Bahati Ngusa (25) nao baada ya kunywa dawa hiyo, walizirai na kukimbizwa katika kituo cha afya kupatiwa matibabu.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Shinyanga, Debora Magiligimba, amethibitisha  kutokea kwa tukio hilo nyumbani kwa mganga huyo aliyefahamika kwa jina la Dela Megejuwa (44).

Chanzo: millardayo.com