Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mtoto wa Simbachawene ahukumiwa

Simba Chaa Mtoto wa Simbachawene ahukumiwa

Wed, 24 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mfanyabiashara, James Simbachawene (24) ambaye ni mtoto wa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), George Simbachawene, amehukumiwa kulipa faini ya Sh250, 000 na kufungiwa leseni yake ya udereva kwa miezi sita baada ya kukiri makosa matatu.

Mshtakiwa huyo amefikishwa mahakamani hapo leo Jumatano Agosti 24, 2022 jioni na kusomewa mashtaka yake na wakili wa Serikali, Daisy Makakala, mbele ya Hakimu Mkazi Aron Lyamuya.

Mashitaka hayo ni pamoja na kuendesha gari kwa hatari, kuendesha gari akiwa amelewa na kuendesha gari bila kuwa na bima.

Baada ya kusomewa mashitaka hayo, Simbachawene alikiri na ndipo hakimu Lyamuya alipoahirisha kesi ili kumwandikia hukumu.

Baada ya muda mfupi, ndipo hakimu Lyamuya alimhukumu Simbachawene kulipa faini ya Sh100,000 kwa kosa la kuendesha gari kwa hatari, Sh100,000 kwa kosa la kuendesha gari akiwa amelewa na Sh50,000 kwa kosa la kuendesha gari bila kuwa na bima.

Pamoja na faini hiyo, leseni ya Simbachawene imefungiwa kwa miezi sita. Awali, Wakili Makakala alidai kuwa mshtakwia anakabiliwa na kesi ya makosa ya Usalama barabara namba 284/2022.

Mshtakiwa anadaiwa kutenda makosa hayo, Agosti 20, 2022 katika barabara ya Haile Selassie, eneo la St Peter, wilaya ya Kinondoni.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live