Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mtoto mwingine auawa Njombe

39696 Njombepic Mtoto mwingine auawa Njombe

Mon, 4 Feb 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Rachael Malekela (7), mwanafunzi wa darasa la pili Shule ya Msingi Matembwe wilayani Njombe ameuawa na mwili wale kutupwa kichakani.

Akizungumza na Mwananchi leo Jumamosi Februari 2, 2019 mwenyekiti wa kijiji cha Matembwe, Brayson Malekela amethibitisha tukio hilo na kubainisha kuwa binti huyo ni mtoto wa mdogo wake.

Amesema wazazi wa mtoto huyo walibaini kutoonekana nyumbani jana saa 12 jioni, walitoa taarifa katika uongozi wa kijiji na wananchi kuanza kumtafuta na saa 4 usiku walikuta mwili wa mtoto huyo katika msitu wa miti mipana uliopo kijijini hapo.

“Huyu mtoto shingoni kama vile amechomwa na vitu vyenye ncha kali, Pia sehemu ya shingo kwa nyuma kama amechomwa na vitu vya nchi kali na katika koromeo kama amekatwa hivi,” amesema Malekela.

Mapema leo asubuhi Mwananchi lilizungumza na mkuu wa wilaya ya Njombe, Ruth Msafiri  na kubainisha kuwa amepata taarifa hizo na kuahidi kuzitolea ufafanuzi.

Saa 6:17 mchana leo Ruth amesema,” Ni kweli mtoto kwa jina ndio huyo na ameuawa nyuma tu ya nyumba yao na kutupwa kwenye shamba la miti.”

Endelea kufuatilia Mwananchi kwa taarifa zaidi



Chanzo: mwananchi.co.tz