Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mtoto atozwa mil 5/- kwa kumtusi mama Instagram

60c27fa5032b37513e926488aa218195 Mtoto atozwa mil 5/- kwa kumtusi mama Instagram

Fri, 24 Jul 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

MKAZI wa Mbuyu Zanzibar, Daurat Salum Suleiman amehukumiwa kulipa faini ya Sh milioni tano au kutumikia kifungo cha miaka miwili jela baada ya kupatikana na hatia ya kumtusi mama yake mkubwa kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram.

Daurat alihukumiwa katika Mahakama ya Ilala jijini Dar es Salaam. Hakimu Mkazi Mfawidhi, Martha Mpaze Na Mwandishi Wetu MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) jana ilitangaza kuwa Mkoa wa Njombe ulikuwa unaongoza kwa hali ya baridi zaidi ya mikoa mingine nchini. Kwa mujibu wa utabiri wa TMA kiwango cha juu cha joto Njombe jana mchana kilitarajiwa kuwa nyuzi joto 14 (14°C).

TMA pia juzi ilitoa utabiri kwamba, kutakuwa na hali mbaya ya hewa kuanzia Julai 22 hadi 26 mwaka huu kwenye ukanda wa pwani ya Bahari ya Hindi ikiwemo mikoa ya Dar es Salaam, Mtwara, Lindi, Tanga na Pwani. Mamlaka hiyo ilitabiri kuwa kwenye maeneo hayo juzi kungekuwa na upepo mkali unaofikia kilomita 40 kwa saa na mawimbi makubwa yanayofikia mita 2.5.

TMA ilitabiri kuwa jana kungekuwa na upepo mkali unaofikia kilomita 50 kwa saa na mawimbi makubwa yanayofikia mita 2.8 kwenye maeneo ya ukanda wa pwani ya Bahari ya Hindi ikiwemo mikoa ya Lindi, Dar es Salaam, Tanga, Mtwara na Pwani ikijumuisha visiwa vya Mafia.

Mamlaka hiyo imetoa angalizo la kuwepo upepo mkali unaofikia kilomita 40 kwa saa kwenye baadhiya maeneo ya Ziwa Nyasa na Ziwa Tanganyika katika mikoa ya Njombe, Ruvuma, Kigoma, Rukwa na Katavi.

TMA imetoa tahadhari ya kuwepo upepo mkali leo unaofikia kilomita 50 kwa saa na mawimbi yanayofikia mita 2.5 kwenye maeneo ya ukanda wa Pwani ya Bahari ya Hindi ikijumuisha mikoa ya Mtwara, Lindi, Dar es Salaam, Tanga na Pwani ikijumuisha visiwa vya Mafia na Unguja na Pemba.

Kwa kesho TMA imetoa angalizo la upepo mkali unaofikia kilomita 40 kwa saa na mawimbi ya mita 2.5 kwa baadhi ya maeneo ya ukanda wa pwani ya Bahari ya Hindi Mtwara, Lindi, Dar es Salaam, Tanga na Pwani ikijumuisha visiwa vya Mafia na visiwa vya Unguja na Pemba.

Kwa Julai 26 TMA imetoa angalizo la upepo mkali unaofikia kilomita 40 kwa saa na mawimbi ya mita 2.5 kwa baadhi ya maeneo ya ukanda wa pwani ya Bahari ya Hindi Mtwara, Lindi, Dar es Salaam, Tanga na Pwani ikijumuisha visiwa vya Mafia na visiwa vya Unguja na Pemba. alisema, upande wa mashitaka ulipeleka mahakamani mashahidi sita kuthibitisha mashitaka ya udhalilishaji kwa njia ya mtandao na kwamba wameweza kuthibitisha mashitaka hayo bila kuacha shaka.

Alisema baada ya kusikiliza mashahidi alibaini maneno aliyoandika mshitakiwa yalikuwa na lengo la kumdhalilisha mlalamikaji Shabaha Said Chondoma maarufu kwa jina la Teacher. Wakati akijitetea Daurat alikanusha madai kuwa alitenda kosa hilo.

“Baada ya kupitia ushahidi wa mashahidi sita na vielelezo, Mahakama inakutia hatiani kwa kumdhalilisha kimtandao Chondoma hivyo, utatakiwa kulipa faini ya Sh milioni tano na akishindwa kulipa fedha hiyo utatumikia kifungo cha miaka miwili jela,” alisema Hakimu Mpaze.

Kabla ya kusomwa hukumu hiyo, Wakili wa Serikali, Gloria Mwenda akisaidiana na Grace Mwanga alidai kuwa hawana rekodi za nyuma za mshitakiwa na ni kosa lake la kwanza. Hata hivyo, aliomba mahakama itoe adhabu kali ili iwe fundisho kwa wengine.

Wakili wa mshitakiwa huyo, Nassoro Hamis aliomba mahakama hiyo impe mshitakiwa adhabu ndogo kwa sababu ni kosa lake la kwanza. Pia alidai mshitakiwa huyo ni mgonjwa na ana watoto watano ambao ni wadogo na kwamba mtoto wa mwisho ana umri chini ya mwaka mmoja hivyo, inahitaji mtu wa kuwahudumia ambaye ni mama.

Ilidaiwa mahakamani kuwa Desemba 28 na 29, 2018 ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Daurat alitumia lugha ya kumdhalilisha Chondoma kwa kutumia mtandao wa kijamii wa Instagram kwa nia ya kumnyanyasa kwa kuposti maneno ya matusi.

Mshitakiwa anadaiwa kuwa alikuwa anachati Instagram na mtoto wa Chondoma (Sharifa Ally), lakini baadaye mshitakiwa alianza kuposti matusi akimtukana mama yake Sharifa ambaye ndiye mlalamikaji katika kesi hiyo namba 490/2019.

Chanzo: habarileo.co.tz