Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mtoto asimulia ‘babu’ miaka 61 alivyombaka

32655 Mtotopic Tanzania Web Photo

Fri, 21 Dec 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Moshi. Wakati Rashid Mohamed Sadick (61) maarufu kama Babu Pipi akihukumiwa kifungo cha maisha jela baada ya kutiwa hatiani kwa kumbaka mtoto mwenye umri wa miaka 11, ushahidi wa mtoto huyo umeacha simanzi.

Katika ushahidi wake, mtoto huyo alidai Machi 2017, Babu Pipi alimtuma mtoto mwingine amuite na walipofika kwa mtuhumiwa alimtuma mtoto huyo mwingine kwenda dukani.

Baada ya kumtuma, mtuhumiwa huyo alimwambia mtoto aliyembaka kuwa anataka awe mchumba wake, lakini mtoto alikataa na kumweleza kuwa yeye bado ni mdogo.

Kwa mujibu wa ushahidi wake, baada ya kumjibu hivyo mshtakiwa alimshika kwa nguvu na kumuingiza chumbani hadi kitandani na kumvua nguo kwa nguvu kisha kumbaka.

Mtoto huyo alidai baada ya mtuhumiwa kumaliza alimpa Sh1,000 na huo ndio ukawa mwanzo wa kumfanyia vitendo hivyo mara kwa mara na kila akimaliza alikuwa akimpa Sh1,000 au pipi. Kabla ya kushtakiwa kwa kosa hilo, 2017 Babu Pipi, mkazi wa Bomambuzi alifunguliwa shauri polisi akituhumiwa kuwabaka wanafunzi watano.

Polisi walilazimika kufunga jalada baada ya uchunguzi wa awali uliofanywa na madaktari kuthibitisha hawakuingiliwa kimwili.

Akitoa hukumu dhidi ya mshtakiwa huyo, Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi, Bernazitha Maziku alisema ushahidi uliotolewa ulikuwa mzito na haukuacha shaka yoyote.

Hakimu aliukataa utetezi wa mshtakiwa kuwa alikuwa akigawa pipi kwa watu wengi, lakini hakuwabaka.



Chanzo: mwananchi.co.tz