Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mtoto aliyepotea Dar, apatikana Arusha

71656 Mtoto+pic

Fri, 16 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mwanafunzi wa darasa la Saba katika shule ya msingi na awali ya Tuwapende, Daniel Evans (12) aliyepotea Agosti 10, 2019 jijini Dar es Salaam amepatikana leo Alhamisi Agosti 15,2019 mkoani Arusha.

Akizungumza kwa simu na Mwananchi, Baba wa mtoto huyo, Evans Rubara amesema mtoto wake anatarajiwa kusafirishwa kesho Ijumaa Agosti 16,2019 kupelekwa Dar es Salaam.

“Sina mengi ninayoweza kueleza zaidi ya kushukuru sana juu ya kupatikana kwake, hatujui ilikuwaje lakini tutakuwa na mengi ya kusema kesho atakapofika,” amesema Rubara.

Awali, alipotembelea ofisi za Mwananchi Agosti 13,2019 Rubara alisema mtoto wake alitoweka katika mazingira ya kutatanisha Agosti 10,2019 nyumbani kwao Bunju, Dar es Salaam huku akiaga nyumbani kuwa amekwenda kucheza.

“Siku hiyo nilikuwa nimeenda shuleni kwao Tuwapende watoto Nursery & Primary katika kikao cha wazazi, kwa sababu yuko darasa la saba tulikuwa tukijadili namna ya kuwasaidia kazi za nyumbani ili waweze kufanya vizuri katika mitihani yao lakini pia kuhusu sherehe yao ya kumaliza elimu ya msingi.”

“Niliporudi nyumbani majira ya saa 6 mchana nilifunguliwa geti na mdogo wangu jambo ambalo si la kawaida kwani Daniel hufanya hivyo siku ambazo yuko nyumbani,” alisema 

Habari zinazohusiana na hii

Jambo hilo lilimfanya kumuuliza mdogo wake sehemu alipo Daniel huku akipewa jibu la kuwa anacheza nje licha ya kuwa ni muda mrefu umepita tangu amuage.

“Tulimuita arejee nyumbani lakini hakuonekana, tukaanza kumtafuta huku na kule bila mafanikio, nikampigia simu mke wangu akasema mtoto hayupo kwake wala ndugu zangu wote nilipowapigia walisema hawajamuona,” alisema

“Ilipofika saa 11 jioni tulitoa taarifa serikali za mitaa, tukatangaza msikitini, tukatoa taarifa polisi lakini bila mafanikio yoyote hadi siku hiyo ya Jumamosi ikawa inaelekea kuisha.”

Alisema usiku huohuo alisambaza ujumbe katika mitandao ya kijamii ikiwemo WhatsApp katika kundi la wazazi wa wanafunzi wa darasa la saba katika shule anayosoma ndipo alipokea simu iliyokuwa ikizungumzia kuonekana kwa Daniel katika eneo la Kerege Bagamoyo

“Niliambiwa Kerege alikwenda nyumbani kwao Hilary ambaye ni mwanafunzi mwenzie sehemu ambayo hata siku moja hajawahi kwenda na hawana mazoea, kilichonishangaza ni pale alipoulizwa namba za simu za wazazi wake kusema hazijui wakati anazifahamu.” Alisema

Eneo la Kerege alipoonekana Daniel ni Kilomita 16.5 kutoka eneo la Bunju analoishi huku baadhi ya watu katika eneo la Mapinga lililopo Kilomita 2.3 kutoka Kerege wakikiri kumuona akizunguka lakini hawajui aliko.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz