Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mtoto afariki kwa kunywa dawa ya mifugo, mwingine anusurika

Mtoto Pic Data Mtoto afariki kwa kunywa dawa ya mifugo, mwingine anusurika

Tue, 4 Jan 2022 Chanzo: www.mwananchi.co.tz

Mtoto mwenye umri wa miaka mitano amefariki dunia huku mwingine akinusurika baada ya kunywa dawa ya chanjo ya ng'ombe katika kitongoji cha Imalamakoye Wilaya ya Urambo mkoani Tabora.

Mwenyekiti wa kitongoji hicho, Michael Phillipo amesema kuwa kifo hicho kimetokea baada ya watoto hao wa familia moja kunywa dawa ya chanjo ya ng'ombe wakidhani ni dawa ya kikohozi.

Amesema mtoto mkubwa mwenye umri wa miaka saba anayesoma darasa la pili alikunywa dawa hiyo kabla ya  kumpa mdogo wake anywe ambaye bahati mbaya alifariki dunia.

Kamanda wa Polisi mmkoani humo, Richard Abwao amethibitisha kutokea kwa tukio hilo akisema mmoja wa watoto hao alikuwa anaumwa kikohozi.

"Mdogo alikuwa anaumwa kikohozi, sasa mkubwa akanywa na kumpa mdogo wake naye anywe na kusababisha kifo chake" ameeleza Kamanda Abwao

Amesema kuwa uchunguzi wa tukio hilo unaendelea na taarifa zaidi itatolewa wakikamilisha uchunguzi huo.

Chanzo: www.mwananchi.co.tz