Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mtendaji wa kijiji afungwa miaka mitano akiwa nje kwa dhamana

24987 Mtendaji+pic TanzaniaWeb

Thu, 1 Nov 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mwanga. Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya Mwanga mkoani Kilimanjaro, Mariamu Lusewa, jana alimhukumu kwenda jela miaka mitano aliyekuwa ofisa mtendaji wa Kijiji cha Lomwe, Mussa Mteti kwa kosa la kughushi muhtasari wa kikao cha kamati ya fedha, uchumi na mipango ya kijiji hicho.

Mteti ambaye aliacha kuonekana mahakamani hapo baada ya utetezi wake akiwa chini ya dhamana, alihukumiwa bila kuwapo mahakamani ambapo hakimu alitoa hati ya kumkamata.

Awali alifikishwa mahakamani hapo na mwendesha mashtaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Suzan Kimaro na kusomewa makosa matatu likiwamo la ubadhirifu.

Akimsomea mashtaka hayo, mwendesha mashtaka huyo aliiambia Mahakama kuwa Mteti alighushi muhtasari wa kikao hicho na kuonyesha kwamba kamati iliridhia na kuidhinisha matumizi ya fedha ya Sh270,000, jambo ambalo si kweli na ni kosa kisheria.

Baada ya hakimu kuridhika na ushahidi uliowasilishwa na Takukuru, katika kosa la kwanza la ubadhirifu alimhukumu Mteti kulipa faini ya Sh2 milioni au kwenda jela miaka mitano.

Katika kosa la pili la ubadhirifu, alihukumiwa kulipa faini ya Sh5 milioni au kifungo cha miaka mitano jela.

Kosa la tatu lililohusu kughushi muhtasari wa kamati ya fedha na uchumi, Hakimu Lusewa alimhukumu Mteti kutumikia kifungo cha miaka mitano jela.

Chanzo: mwananchi.co.tz