Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mtendaji wa kata kortini kwa tuhuma za rushwa

RUNGU Mtendaji aliomba rushwa ya laki tatu kwa mzazi mwenye mtoto mtoro

Thu, 28 Apr 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) imemfikisha mahakamani Ofisa Mtendaji wa Kata ya Nkinga wilayani Igunga, Salama Habibi Ziada kwa tuhuma za kuomba na kupokea rushwa kwa mzazi ambaye mtoto wake alikuwa mtoro shuleni.

Mtendaji huyo amefikishwa mbele ya Mahakama ya Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Igunga, Jackline Kessy leo Alhamisi Aprili 28, 2022.

Mwendesha mashtaka wa Takukuru kutoka Wilaya ya Nzega, Mazengo Joseph ameiambia mahakama kuwa katika shtaka la kwanza, mshtakiwa huyo Novemba 6, 2021 katika Kijiji cha Ilunga, kata ya Nkinga, aliomba rushwa ya Sh300,000 kutoka kwa Ndulu Seni Darishi, ili asimchukulie hatua mzazi huyo aliyekuwa na mtoto wake ambaye hakuwa akienda shuleni katika sekondari ya Nkinga akiwa kidato cha pili.

Mazengo amedai kuwa katika shtaka la pili, mshtakiwa alipokea rushwa Novemba 6, 2021 ya Sh280,000 kutoka kwa mzazi huyo.

Mwendesha mashtaka huyo amesema mshtakiwa ametenda makosa hayo mawili kinyume na kifungu 15(1)a cha Kuzuia na Kupambana na Rushwa namba 329 mapitio ya mwaka 2019 inayozuia kutenda makosa kama hayo.

Baada ya kusomewa mashitaka hayo mbele ya Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo, Jackline Kessy, mshtakiwa hakutakuwa kujibu chochote kwa kuwa Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo hana mamlaka ya kusikiliza shauri hilo.

Advertisement Mwendesha mashtaka Mazengo Joseph ameiambia mahakama kuwa upelelezi wa kesi hiyo umekamilika na Hakimu kuiahirisha Hadi Mei 23, 2022 na mshtakiwa yupo nje kwa dhamana ya Sh5.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live