Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mtendaji wa Kijiji jela miaka 20 kwa ubadhirifu

Kortini Geita.jpeg Mtendaji wa Kijiji jela miaka 20 kwa ubadhirifu

Fri, 28 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama ya Wilaya ya Mbulu imemtia hatiani aliyekuwa Mtendaji wa Kijiji cha Kainam, Samwel Qambina Dukho kwa mashtaka ya Ubadhirifu, Matumizi Mabaya ya Madaraka na Wizi katika Utumishi wa Umma.

Amehukumiwa Miaka 20 jela kwa Kosa la Kwanza, Miaka 20 kwa Kosa la Pili na mwaka mmoja kwa Kosa la Tatu, ambapo atatumikia adhabu zote kwa pamoja.

Pia ameamriwa kurejesha Tsh. 3,687,000/= ambazo alizifanyia ubadhirifu au mali yake iuzwe ili kufidia deni hilo

Chanzo: www.tanzaniaweb.live