Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mtendaji wa Kata atupwa jela miaka 20 kwa ufujaji wa fedha

Law 1063249 1920 A35e082d75c748e18bf8108733914dc1 660x400 Mtendaji wa Kata atupwa jela miaka 20 kwa ufujaji wa fedha

Fri, 26 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Agosti 24, 2022 Jamhuri imeshinda katika Shauri Na. ECO. 90/2020 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha.

Shauri hili lilimhusu, JULIUS K. MBISE, aliyeshtakiwa kwa makosa ya Ufujaji na Ubadhirifu, Matumizi Mabaya ya Madaraka pamoja na Kuisababishia Serikali Hasara, kinyume na vifungu vya 28 (1), 31 vyote vya PCCA, Cap 329 na aya ya 10 (1) ikisomwa pamoja na Jedwali la kwanza la Sheria ya EOCCA, Cap 200 [R.E 2019].

Mshtakiwa ambaye ni Afisa Mtendaji wa Kata ya KIKWE, alifuja kiasi cha sh Milioni Saba (7,000,000/=) fedha za Halmashauri ya (W) ya Meru.

Mshtakiwa amepatikana na hatia na amehukumiwa kutumikia kifungo cha miaka 20 Jela na kutakiwa kurejesha kiasi cha sh. Milioni Saba (7,000,000/=) alizofuja.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live