Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mtanzania anaswa Afrika Kusini na dawa za kulevya

15131 Pic+mtanzania TanzaniaWeb

Sun, 2 Sep 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mtanzania Richard Andrew Hao (42) amekamatwa nchini Afrika Kusini akidaiwa kuwa na kilo 1 za dawa za kulevya aina ya heroin alizozificha kwenye gari yake ya kutembelea.

Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za kulevya nchini (DCEA), Rogers Siyanga amesema leo Septemba 2, 2018 kuwa mtuhumiwa alikamatwa jana eneo la Durban nchini humo akiwa na dawa hizo ambazo zilikuwa kwenye gari lake.

Amesema mtuhumiwa huyo alikuwa na hati yake ya kusafiria yenye namba AB408563 amekuwa akitumiwa na wafanyabishara wakubwa kusafirisha na kuzisambaza nchi mbalimbali.

“DCEA tunaendelea kuchunguza ili tujue hapa nchini anatokea mkoa na sehemu gani itakapojulikana tutawajulisha. Pia mtuhumiwa huyo bado anashikiliwa na vyombo vya ulinzi wa nchi hiyo kwa ajili ya uchunguzi zaidi na ukikamilika hatua za kisheria zitachukuliwa,” amesema Siyanga.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz