Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mtanzania akutwa na hatia ya ugaidi Kenya

63564 Mtanzaniapic

Thu, 20 Jun 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Nairobi, Kenya. Raia wa Tanzania, Rashid Mberesero amekutwa na hatia kutekeleza shambulio la kigaidi nchini Kenya mwaka 2015.

Mtanzania huyo mwenyeji wa Kilimanjaro pamoja na Wakenya wawili wamepatikana na hatia ya kuhusika katika shambulio la la ulipuaji wa Chuo Kikuu cha Garissa na kusababisha mauaji ya wanafunzi 148.

Washtakiwa hao wamekutwa na hatia ya kufanya njama za kutekeleza ugaidi na kuwa wanachama wa kundi la kigaidi la Al Shabaab lenye makao yake makuu nchini Somalia.

Wengine walipatikana na hatia ni pamoja na Hassan Edin na Mohammed Abdi anayefahamika kwa jina lingine la Mohamned Ali Abikar.

Hata hivyo, mahakama hiyo ili muondoa katika mashtaka mtu wa nne Sahal Diriye Hussein.

Hatima ya watuhimiwa hao itajulikana Julai 3, mahkama hiyo itakapotoa uamuzi wake.

Pia Soma

Awali ilidaiwa mahakamani hapo kuwa shambulio hilo lilitekelezwa na kundi la Al-Shabab kwa kushirikiana na lile la Al-Qaeda katika chuo hicho kilichopo Kaskazini Mashariki mwa Kenya.

Hili ni shambulio pili kubwa kutokea katika historia ya Kenya. Mwaka 1988 zaidi ya watu 200 walifariki dunia baada shambulio la kigaidi lilofanywa katika ofisi za ubalozi wa Marekani.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz