Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mtanzania akamatwa na madawa ya kulevya Sauz

MTANZANIA AKAMATWA Mtanzania akamatwa na madawa ya kulevya Sauz

Fri, 23 Dec 2022 Chanzo: millardayo

Mamlaka ya kupambana na Dawa za Kulevya nchini Afrika Kusini imetangaza kumkamata Mtanzania Ahmadi Mbwana Chonde (50) akiwa na kilo mbili za dawa za kulevva aina ya heroin, Mamlaka ya kudhibiti dawa za kulevya Tanzania imethibitisha.

Taarifa iliyotolewa na Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini Tanzania (DCEA) imesema kuwa Chonde mwenye hati ya kusafiria yenye namba TAE145658 alikamatwa katika uwanja wa ndege wa jijini Cape Town Jumanne December 20, 2022.

Taarifa hiyo ya DCEA imesema kuwa Chonde alikua kaficha dawa hizo za kulevya ndani ya sanduku lake la nguo alilokuwa akisafiri nalo kutoka Cape Town kuelekea nchini India katika miji ya Kochi na Chennai kupitia Doha, Qatar.

Chanzo: millardayo