Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mtangazaji ITV auawa, mwili watupwa Mwenge

Af2d26666cff6dfff1b30ab6ac289564 Mtangazaji ITV auawa, mwili watupwa Mwenge

Mon, 29 Mar 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

JESHI la Polisi Mkoa wa Kinondoni limethibitisha kifo cha utata cha mfanyakazi wa kituo cha televisheni cha ITV, Blandina Sembu (47).

Blandina alikuwa mtangazaji wa kipindi cha Jarida la Wanawake. Kwa mujibu wa polisi watu wasiojulikana waliutupa mwili wa Blandina saa 5.30 usiku wa kuamkia jana Machi 28.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kinondoni, ACP Ramadhan Kingai, alisema watu hao walisimama kwa muda jirani na baa ya Maryland iliyopo Mwenge, Dar es Salaam na kuutupa mwili huo kando ya barabara.

Kwa mujibu wa Kamanda Kingai watu waliotupa mwili wa Blandina walikuwa na gari jeusi aina ya Noah.

"Jeshla la Polisi limeanza uchunguzi wa tukio hilo ili kubaini chanzo chake na wahusika ili waweze kuchukulìwa hatua za kisheria," alisema.

KATIKA HATUA NYINGINE: Jeshi la Polisi limekamata watu wanane kutoka eneo la Kariakoo kwa tuhuma za kuhusika na vitendo vya ubadilishaji wa namba za usajili wa simu (IMEI) zikiwemo simu zinazohusika katika uhalifu.

Akizungumza kuhusu tukio hilo, ACP Kingai alisema watuhumiwa walikamatwa katika mitaa ya Aggrey na Likoma iliyopo katika eneo hilo la Kariakoo jijini Dar es Salaam.

Alisema watuhumiwa hao wapo mahabusu wakati upelelezi wa ukiendelea.

Chanzo: www.habarileo.co.tz