Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mtandao wa wezi wa pikipiki Dar kwa kutumia mjamzito feki wanaswa

Screenshot 20220402 085901 Twitter Mtandao wa wezi wa pikipiki Dar kwa kutumia mjamzito feki wanaswa

Sat, 2 Apr 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam wamemkamata Mohamed Omary (27), mkazi wa Chamazi kwa tuhuma za kushiriki katika matukio ya unyang’anyi wa Pikipiki kwa waendesha Bodaboda kwa kushirikiana na wenzake, Athuman Abdallah (29) mkazi wa Yombo na Hassan Twaha maarufu Dangote ( 21) Mkulima wa Mtongani Temeke

"Mbinu ambayo wahalifu hao wamekuwa wakiitumia katika unyang’anyi wa Pikipiki hizo ni kumtumia Mwanamke mmoja ambaye hujifanya mjamzito aliyefahamika kwa jina la Aziza Hamza (21), Mkazi wa Yombo ambaye hukodi bodaboda mpaka walipo wenzake kwa ajili ya kupora pikipiki"

"Tukio la uporaji likikamilika wahalifu hao huzipeleka pikipiki hizo kwa Omary Salum (30) , mkazi wa Tandika, Kilimahewa ambaye kazi yake ni kutoa GPRS/ ving’amuzi kwa pikipiki zenye ving’amuzi, Athuman Mohammed Bakari maarufuku BOKO ( 42) mkazi wa Kilwa Kivinje yeye hujihusisha na kuzitafutia kadi na kuziuza katika mikoa ya Mtwara na Lindi"

"Jeshi la Polisi limefanikiwa kumkamata Sophia Musa (28) mkazi wa Toangoma ambaye ndiye mpokea maombi ya kutengeneza kadi toka kwa BOKO na baadae kumpelekea Ibrahimu Ally (31) mkazi wa Buguruni ambaye hufanya kazi ya kudurufu kadi hizo za Pikipiki, katika katika upekuzi watuhumiwa hao wamekutwa na Pikipiki tatu (3) za wizi, (MC 292 DCE, MC 733CEG na MC 250 DBF), kadi za pikipiki (9) Kadi za Gari (11), vyeti vya kuzaliwa, vyeti vya kumaliza elimu ya sekondari, stika za mamlaka ya mapato (TRA) na stika za Baraza la Mitihani vyote vinachunguzwa..."

Chanzo: www.tanzaniaweb.live