Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mtandao wa matapeli wa viwanja wanaswa

7ba7b3f0a29bbb123420d78e21836718 Mtandao wa matapeli wa viwanja wanaswa

Thu, 26 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Polisi mkoani Morogoro inawashikilia watu 16 kwa tuhumza za kujihusisha na utapeli wa kuuza viwanja kwa mtu zaidi ya mmoja wakitumia nyaraka za kugushi na kugonga mihuli bandia ili kutekeleza uhalifu wao na kujipatia mamilioni ya fedha .

Kamanda wa Polisi wa mkoa huo ,Fortunatus Musilimu amesema hayo leo Mei 25, 2022 wakati akizungumza na waandishi wa habari ya kwamba watuhumiwa hao walikamatwa kwa nyakati tofauti kuanzia jana Mei 24, 2022.

Amesema watuhumiwa hao wamekuwa wakishirikiana na viongozi mbalimbali wasiowaadilifu wa maeneo husika kupima viwanja katika mashamba yasiyokuwa yao, kuandaa mihtasari feki na hati bandia za umiliki na uuzaji wa viwanja na mashamba hayo.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo amesema, watuhumiwa hao wamekuwa wakishirikiana na watendaji wa Taasisi, Mamlaka, na Idara mbalimbali za serikali katika kutenda uhalifu huo.

Amesema watuhumiwa hao wamekuwa kero na kuzua taharuki katika jamii na kusababisha kutokea kwa uvunjifu wa amani na wamekuwa wakishirikiana na wahalifu wenzao kutoka nje ya mkoa wa Morogoro kufanya uhalifu huo na kuondoka.

Musilimu ametoa angalizo kwa kuwataka wote wanaojihusisha na utapeli wa viwanja na mashamba mkoani Morogoro kuacha mara moja kwani hawatakuwa salama.

“ Wote waliojihusisha katika utapeli wa viwanja na kutoroka au kuhama wajue kwamba watatafutwa huko walipo na kutiwa mbaroni na kurejeshwa kujibu tuhuma zao …ni vyema wakajisalimisha wenyewe badala ya kusubiri kutafutwa” ameonya Kamanda Musilimu

Amesema kuwa Polisi itaendelea kuhojiana nao ili kubaini mtandao mzima na hivyo kuwataka wote ambao waliwahi kutapeliwa viwanja vyao kufika Kituo cha Polisi cha Kati (Central Morogoro) ili kuwatambua watuhumiwa hao kwa hatua za kisheria.

Musilimu amesema ,wale wote ambao kesi zao zipo Mabaraza ya Ardhi na Mahakamani ambao wametapeliwa na watuhimiwa hao kufika kuwatambua na hata wale wote ambao walitapeliwa na kukosa haki na kusamehe kwa kumuachia Mungu wafike ili wapate haki yao.

“ Hakuna tapeli atakayeachwa , kila jiwe litaguswa “ meonya Kamanda Musilimu

Chanzo: www.tanzaniaweb.live