Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mtaalamu feki wa maabara anaswa Rombo

59181 Fekipic

Wed, 22 May 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Rombo. Mtaalamu feki wa maabara anaswa akitoa huduma za maabara katika zahanati ya Mkuu iliyopo Rombo Mkoani Kilimanjaro.

Mtaalam huyo aliyejulikana kwa jina la Peter Mturi, amenaswa leo Jumatano Mei 22, 2019 na maofisa wa Baraza la wataalamu wa maabara nchini, walipokuwa wakiendelea na kazi ya uhakiki wa usajili wa wataalamu hao mkoani humo.

Akizungumzia kunaswa kwa mtu huyo,  Naibu msajili wa baraza hilo, Vera Nelson amesema hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake kutokana na huduma aliyokuwa akitoa kwa Watanzania si sahihi na kwakuwa hajasomea taaluma hiyo.

Amesema kwa siku kijana huyo alikua akihudumia wagonjwa kati ya 30 hadi 40 na majibu aliyokuwa akiwapa wagonjwa si ya kweli.

“Tuko hapa mkoani Kilimanjaro tunafanya kazi ya uhakiki wa wataalamu wetu wa maabara, lakini tumebaini uwapo wa mtaalamu feki ambaye ana leseni feki za maabara, huyu kijana tuliyemkuta katika zahanati hii hajulikani amesomea wapi na leseni aliyonayo ya maabara ni feki.

“Huyu kijana tangu aingie katika zahanati hii ni miezi minne, atakuwa ameumiza Watanzania wangapi? tutachukua hatua za kisheria dhidi yake na tutamfikisha katika vyombo  husika,” amesema.

Pia Soma

 

 

Badaa ya kubaini kuwa mtaalamu huyo hana sifa, Nelson amesema wamesimamisha huduma za kituo hicho hadi mmiliki atakapopata mtaalamu mwingine mwenye sifa.

 

Akizungumzia hilo, Msimamizi wa Huduma za Maabara na Mkaguzi wa Mkoa wa Kilimanjaro, Faustine Shayo amesema huduma za maabara mkoani humo zinaridhisha, lakini wako baadhi ya watu wachache  ambao si waaminifu wanaharibu tasnia hiyo.

 

“Kutokana na uwepo kwa watu ambao sio wataalamu katika vituo vyetu vya afya vinafanya watu wanapata majibu ambayo si sahihi na hii inasababisha mgonjwa kupoteza maisha au kukaa hospitali kwa muda mrefu kwa kupewa tiba ambayo si sahihi  kutokana na majibu yaliyotolewa maabara na mtu ambaye si mtaalam,” amesema Shayo.

 

 

Chanzo: mwananchi.co.tz