Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mstaafu wa Polisi ajinyonga bafuni

Ajinyonga Pc Data Mstaafu wa Polisi ajinyonga bafuni

Wed, 26 Jan 2022 Chanzo: www.mwananchi.co.tz

Mstaafu wa Jeshi la Polisi nchini, Omary Charema Msangi amejiua kwa kujinyonga bafuni kwake kwa kutumia waya wa pasi.

Tukio la kujinyonga mstaafu huyo limetokea usiku wa kuamkia jana akiwa kwenye nyumba aliyokuwa akiishi eneo la Kiboriloni Manispaa ya Moshi ambapo mwili wa mstaafu huyo ulichukuliwa na kupelekwa kuhifadhiwa Hospitali ya Rufaa ya KCMC.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa  amethibitisha kutokea kwa  tukio leo Jumatano Januari 26, 2022 akisema bado wanaendelea na uchunguzi wa kubaini chanzo cha kujinyonga kwa mstaafu huyo.

"Ni kweli hili tukio limetokea na tunafuatilia kujua hasa chanzo cha kujinyonga kwake," amesema Kamanda Maigwa

Taarifa za chanzo cha  kijinyonga kwa  askari huyo kutoka kwa mmoja wa ndugu wa familia hiyo zinadai kuwa wakati mwanaume huyo akiwa kwenye matibabu mkoani Dar es salaam, mke wake alitumia nafasi hiyo kuuza mali zake zote ikiwa ni nyumba, mashamba pamoja na mali nyingine.

Inadaiwa kuwa baada ya mtaafu huyo kurejea nyumbani kutoka kwenye matibabu alikuta nyumba yake imeuzwa na kulazimika kwenda kupanga.

Mwili wa mwanaume huyo unatarajiwa kuzikwa leo  Usangi Wilaya ya Mwanga.

Chanzo: www.mwananchi.co.tz