Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Msofe wezake waachiwa huru

404073edee0e366023c0cd2a595b58bc.jpeg Msofe wezake waachiwa huru

Fri, 18 Jun 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

MFANYABIASHARA maarufu, Marijan Msofe (55) alimaarufu, Papa Msofe na wenzake wameachiwa huru baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) Sylvester Mwakitalu kuondoa hati ya mashtaka mahakamani.

Msofe alikamatwa na kupandishwa kizimbani Disemba 2019 na wenzake akiwemo Mfanyabiashara Fadhili Mganga, Wenceslau Mtui, Josephine Haule na Wakili wa Kujitegemea Mwesigwa Mhingo (38) wakikabiliwa na mashtaka matono yakiwemo tuhuma za kutakatisha Dola za Malekani 410,000.

Kati ya washtakiwa hao, Mganga alitumikia kifungo cha nje kufuatia hukumu ya mwaka 2020. Msofe na wezake wengine waliendelea kusalia mahabusu wakituhumiwa na makosa ya uhujumu uchumi. Hukumu ya Mwaka juzi ilihusu makosa ya udanganyifu ambapo Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu iliwataka kulipa fidia ya Shilingi milioni 70 na kutumikia kifungo cha nje.

Chanzo: www.habarileo.co.tz