Dar es Salaam. Aliyekuwa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi na wenzake wameshindwa kuanza kujitetea kutokana na Wakili wa utetezi, Richard Rweyeongeza kufiwa na mkwe wake.
Mbali na Malinzi, washtakiwa wengine ni aliyekuwa Katibu wa TFF, Mwesigwa Selestine, mhasibu wa shirikisho hilo, Nsiande Mwanga na karani Flora Rauya
Wakili wa Takukuru, Leonard Swai ameieleza mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo Jumanne Agosti 6, 2019 kuwa shauri hilo lilikuja kwa ajili ya kusikiliza upande wa utetezi .
Baada ya maelezo hayo wakili wa utetezi, Richard Rweyeongeza amedai kuwa amefiwa na mkwe wake maiti ipo nyumbani, hawezi kuendelea na utetezi licha ya kukiri kumuandaa mshtakiwa wa kwanza ambaye ni Malinzi.
"Nina msiba maiti ipo ndani kwangu sitaweza kuendelea na utetezi hivyo ninaiomba Mahakama hii iahirishe shauri hili hadi wiki ijayo," amedai Rweyeongeza.
Hakimu Mkazi Mkuu, Maira Kasonde aliahirisha shauri hilo hadi Agosti 13, 2019 itakapokuja kwa ajili ya Malinzi kujitetea.
Pia Soma
- Wataalam wa anga Tanzania waanza uchunguzi ajali ya ndege iliyoua wawili
- Pinda awataka Ma RC wengine kwenda kujifunza kwa Mtaka
- Alichokisema dada wa aliyefariki baada ya kupata ajali na gari ya RC