Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mshtakiwa mwingine aongezwa kesi ya kina Kisena

Kisena' Washtakiwa wakiwa kizimbani

Mon, 23 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkurugenzi wa Maxcom Afrika, Juma Furaji (48) ameunganishwa katika kesi inayomkabili Mkurugenzi wa Udart, Robert Kisena na wenzake watatu wanaokabiliwa na mashtaka 22 likiwemo la kuisababishia hasara Serikali ya Sh4.5 bilioni.

Mshtakiwa huyo alisomewa mashtaka hayo leo Jumatatu Mei 23, 2022 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mfawidhi, Godfrey Isaya wakati shauri hilo lilipokuja kwa ajili ya kutajwa.

Washtakiwa wengine ni Charles Newe (48) Mkurugenzi wa Udart na Mtunza fedha, Tumaini Kulwa (44).

Washtakiwa hao wanaokabiliwa na mashtaka 22 yakiwamo ya utakatishaji fedha, kuongoza genge la uhalifu na kuisababishia Serikali hasara.

Wakili wa Takukuru, Imani Nitumie akimsomewa mashtaka sita yanayomkabili mshtakiwa Furaji alidai kati ya mashtaka hayo manne ni ya utakatishaji wa fedha, moja la kuongoza genge la uhalifu na kuisababishia Serikali hasara

Nitumie alidai kati ya Agosti Mosi na Desemba 30, 2015, Kisena, Furaji na wenzake watatu wanadaiwa waliongoza genge la uhalifu ndani ya mkoa wa Dar es Salaam na kujipatia Sh4, 505,125,000 kutoka Mradi wa Usafirishaji Dar es Salaam (DART) na kwamba hizo fedha zilikuwa katika akaunti ya mradi huo iliyopo benki ya NMB tawi la Benki House.

Advertisement Alidai katika shtaka la utakatishaji  Novemba 18, 2015 katika Jiji la Dar es Salaam kwa nia ovu alihamisha Sh1.1 bilioni kutoka akaunti ya benki ya Internation Commercial kwenda kwenye akaunti ya Kisena huku akijua ni kosa la kughushi.

Katika shtaka lingine kati ya Novemba 19, 2015 katika benki hiyo mshtakiwa huyo alihamisha Sh1.2 bilioni mali ya Maxcom Afrika kwenda kwenye akaunt ya mshtakiwa Kisena wakati akijua ni kosa la kugushi.

Nitumie alidai kati ya Novemba 19, 2015 mshtakiwa huyo alihamisha kiasi cha Sh829.5 milioni kutoka kwenye akaunti ya Maxcom Afrika kwenda kwenye akaunti ya mshtakiwa huyo iliyokuwa benki ya Internation Commercial.

Alidai kati ya Novemba 27, 2015 mshtakiwa huyo akiwa jijini Dar es Salaamkwa kwa lengo la kuficha uhalifu alihamisha kiasi cha Sh1.1 bilioni mali ya Maxcom Afrika akaihamisha kwenye akaunti yake ya benki ya Internation Commercial.

Katika shtaka la kuisababishia hasara Serikali kati ya June Mosi, 2015 na mwaka 2016 Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam washtakiwa wote wanne wakiwa na nia ovu walisababishia hasara UDART kiasi cha Sh4.5 bilioni.

Wakati huo huo Katika kesi ya pili inayomkabili Kisena, Newele, Kulwa na mfanyabiashara, John Samangu (66) upande wa Jamuhuri umedai kuwa wanawasilisha mashtaka Mahakama Kuu.

Washtakiwa hao wanaokabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi namba 20/2022 yenye mashtaka 15 yakiwemo ya kuisababishia UDART hasara Sh750 milioni.

Wakili wa Takukuru, Imani Nitumie alidai shauri lilikuja kwa ajili ya kutajwa na upelelezi umekamilika hivyo aliiomba mahakama hiyo iwapewe muda waweze kuwasilisha mashtaka hayo Mahakama Kuu.

Kesi hizo zimeahirishwa hadi June 6, 2022 kwa ajili ya kutajwa

Chanzo: www.tanzaniaweb.live