Dar es Salaam. Fabian Ishengoma, mshtakiwa kwa kwanza katika kesi ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu inayowakabili mawakala 10 wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), ameuomba upande wa mashtaka kueleza ulipofikia upelelezi wa kesi hiyo.
Mshtakiwa huyo ameeleza hayo leo Jumatatu Mei 20, 2019 katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi, Maira Kasonde baada ya wakili wa Serikali, Janet Magoho kueleza jalada la shauri hilo lipo kwa mwanasheria kwa ajili ya kufanyiwa kazi.
"Wiki mbili zilizopita tuliambiwa jalada liko ofisi ya mwanasheria na leo tumeelezwa hivyo tunaomba kujua upelelezi umefikia wapi miongoni mwetu tuna watoto wadogo na kesi yetu haina dhamana,” amedai Ishengoma.
Wakili Magoho alieleza kuwa wapo katika hatua za mwisho kuandaa ripoti wanachosubiri ni taarifa ya hasara iliyotokea ATCL.
Hakimu Kasonde ameahirisha kesi hiyo hadi Juni 3, 2019 itakapotajwa tena.
Mbali na Ishengoma washtakiwa wenginekatika kesi hiyo ni Adamu Kamara, Mlon Masubo, Alexander Malongo, Tunu Kiluvya, Jobu Mkumbwa, Mohamed Issa, Godfrey Mgomela, Absalom Nyusi na Janeth Lubega.
Pia Soma
- RC Kigoma adai madiwani wanakwamisha miradi ya maendeleo
- Ujenzi wa chelezo, meli mpya ziwa Victoria wafikia asilimia ilimia 30
- 1,637 waajiriwa Zanzibar mwaka 2017/18