Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mshtakiwa adai hajawahi kumbembeleza mpenzi wake warudiane

HUKUMU Mshtakiwa adai hajawahi kumbembeleza mpenzi wake warudiane

Wed, 24 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mshtakiwa Ally Balanda maarufu Idofolo (52) ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa maelezo yaliyopo kwenye nyaraka ya ulinzi wa amani zilikuwa 19 kati ya hizo alisaini karatasi mbili na nusu zilizobaki siyo sahihi ya kwake.

Inadaiwa kuwa mshtakiwa huyo alimuua kwa kisu mpenzi wake Selan Kondo aliyekuwa mwalimu wa shule ya Msingi Tabata.

Balanda akitoa ushahidi huku akiongozwa na Wakili wake wa utetezi, Roman Lamwai alidai kuwa alipofikishwa kwa mlinzi wa amani katika Mahakama ya Mwanzo ya Buguruni alisaini karatasi mbili na nusu lakini kuanzia ukurasa wa nne hadi 19 hakuwahi kusomewa maelezo na sahihi zinazoonekana siyo za kwake.

"Katika nyaraka za mlinzi wa amani nilisaini karatasi mbili na nusu lakini kuanzia ya nne hadi 19 Saini zilizowekwa siyo za kwangu nachokumbuka siku hiyo nilikuwa na uvimbe kwenye jicho lililotokana na kipigo mlinzi alinihoji kidogo na kuniambia niondoke kutokana na kuumwa kwangu," amedai mshtakiwa huyo.

Hata hivyo katika nyaraka alizozikataa mshtakiwa huyo yalikuwa na maelezo yakisema kuwa alinunua kisu ambacho alikinoa na alitembea nacho kwa siku tatu mfululizo Kwa ajili ya kumvizia mpenzi wake.

Pia mshtakiwa huyo alidai kisu na kitambaa kilichotolewa mahakamani hapo kama ushahidi hakina umiliki wake na vielelezo hivyo aliviona kwa mara ya kwanza wakati ulipotolewa ushahidi.

Mshtakiwa huyo alidai kwenye gwaride la utambulizi hakuwahi kufanyiwa na kwenye maelezo ya askari polisi Haruna Mmali inaonyesha alifanyiwa lakini hakufika mahakamani kutokana ushahidi wake.

Alidai anachokumbuka alifikishwa katika kituo cha polisi cha Tabata ambapo alipigwa kisha alipewa nyaraka yenye maelezo alisaini kwa kulazimishwa hivyo ameiomba Mahakama hiyo imwachie huru.

Baada ya maelezo hayo Hakimu Mkazi Mkuu, Franco Kiswaga aliahirisha shauri hilo hadi Juni 28, 2023 Kwa ajili ya hukumu.

Katika kesi ya msingi inadaiwa kuwa Mei 6, 2019 eneo la Tabata Liwiti mshtakiwa huyo alimuua mpenzi wake, Selani Kondo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live