Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mshitakiwa kesi ya Sabaya aomba simu ajitetee

F5b6ae58288b6ab022a6988b0097658f Mshitakiwa kesi ya Sabaya aomba simu ajitetee

Wed, 9 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mshitakiwa wa tatu Watson Mwahomange (39 katika kesi ya Uhujumu Uchumi inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya, ambaye anajitetea mwenyewe baada ya wakili wake, Fridolini Bwemelo kujitoa leo kabla ya yeye kuanza kujitetea, ameiomba Mahakama kuiamuru Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoani Arusha, kupewa simu yake ya kiganjani inayoshikiliwa na taasisi hiyo, ili iwe moja ya kielelezo katika utetezi wake.

Waendesha Mashitaka wa serikali wakiongozwa na Mwendesha Mashitaka Mwandamizi wa serikali, Ofmedy Mtenga walidai hawana pingamizi na hilo, ila mawakili wa Sabaya, Mosses Mahuna na Faudhia Mustapher walipinga ombi hilo na kumtaka mshitakiwa kutoa ushahidi wake bila hiyo simu.

Naye Wakili Ngemela anayewatetea washitakiwa wa tano, sita na saba aliunga mkono hoja za Mahuna na Mstapher na kudai kuwa kuanza kuhitaji simu sasa ni kuisumbua mahakama na kuiomba mahakama hiyo kutupilia mbali hoja hiyo na shahidi aendee kutoa ushahidi.

Hakimu Patricia Kisinda alisema kuwa uamuzi wa hoja hiyo atautoa kesho na aliwaomba mawakili wa utetezi kumpandisha shahidi mwingine kujitetea, ndipo alipopanda Jackson Macha (30) kama shahidi wa tano wa utetezi.

Mbali ya Sabaya washitakiwa wengine katika kesi hiyo ni pamoja na Enock Mnkeni (41) ,Watson Mwahomange (27) maarufu kwa jina la Malingumu, John Aweyo(45), Syliverster Nyegu (26) maarufu kwa jina la Kicheche, ambaye pia ni Msaidizi wa Sabaya, Jackson Macha (29) na Nathan Msuya (31).

Chanzo: www.tanzaniaweb.live