Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mshitakiwa adai kuponzwa na mwanamke aliyekutana naye Mliman City

Hukumu Pc Data Mshitakiwa adai kuponzwa na mwanamke aliyekutana naye Mliman City

Fri, 4 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

MSHITAKIWA Bogias Augustine na wenzake wawili wanakabiliwa na mashitaka matatu ikiwemo unyang’anyi kwa kutumia silaha na wizi.

Hata hivyo, Augustine amedai kuwa hakufanya makosa hayo bali alisingiziwa baada ya kuhusishwa kuwa na mahusiano na mwanamke aliyekutana naye Mlimani City.

Mshitakiwa huyo alidai hayo jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Ferdnadri Kiwonde wakati akitoa utetezi wake. - Agustino alidai kuwa anaamini alifanyiwa utaratibu wa kukamatwa na mlalamikaji kwani askari waliohusika kumkamata hawakutoa taarifa ya ukamatwaji wake wala hakukuta mashitaka yoyote kituoni. - "Nakumbuka kuna siku nikiwa Mlimani City nilikutana na mwanamke aliyedai ananifananisha na tukabadilishana namba wakati tumesimama alitokea mwanaume mmoja ambaye alimwangalia kwa ghadhabu na kumuamuru mwanamke huyo waondoke," alidai Agustino. - Alidai kuwa Februari 18, 2022 akiwa nyumbani kwake walifika askari na kumkamata na kufanya upekuzi ndani ya nyumba yake na kumchukua kumpeleka Kituo cha Polisi Kijitonyama. - Alidai kuwa alikaa kituoni hapo hadi Februari 23, 2022 siku hiyo alikuja askari na kumtaka waende Kituo cha Polisi Oysterbay na walipofika walikuja wanaume wanne ambao kati yao alimtambua mmoja wao kuwa ndiye aliyekutana naye Mlimani City, wakati akizungumza na mwanamke huyo na askari huyo alimwambia atamshikisha adabu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live