Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mshauri wa wafanyabiashara Manyara haitiani kwa kughushi nyaraka

Mshauri Wa Wafanyabiashara Manyara Haitiani Kwa Kughushi Nyaraka Mshauri wa wafanyabiashara Manyara haitiani kwa kughushi nyaraka

Tue, 26 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama ya Hakimu Mkazi Manyara imemhukumu Bw. Ramadhan Rashid Msangi ambaye ni Mshauri wa Wafanyabiashara na mwajiriwa wa Chama cha wenye viwanda na kilimo Mkoa wa Manyara (Bussines Consultant -TCCIA Manyara).

Mshtakiwa huyo ameamriwa na mahakama kulipa faini kiasi cha shilingi 900,000/= au kwenda jela miaka mitatu, kwa kosa la kughushi nyaraka za malipo.

Hukumu hiyo dhidi ya Ramadhani Rashid Msangi ni katika shauri la uhujumu uchumi Na. 05/2023 ambalo lilikuwa linamkabili

Hukumu hiyo imetolewa na Mhe. Martin Massao, Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Manyara Machi 22, 2024.

Mshtakiwa alighushi nyaraka mbali mbali katika marejesho yake kuonesha kuwa alihudhuria na kuendesha mafunzo ya wajasiriamali yaliyofanyika wilayani Hana’ng kwa kipindi cha Mwezi Februari na Juni Mwaka 2018 na kwamba alitumia kiasi cha shilingi 6,695,000/= kugharamia posho ya chakula, ukumbi na nauli kwa waliodaiwa kushiriki mafunzo hayo – huku akijua taarifa hizo hazikuwa sahihi.

Mshitakiwa huyo amelipa faini na kuachiwa huru na mahakama.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live