Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mrundi auawa Kigoma akitaka kupora kwa AK 47

Kamanda Manyama Kigoma Kamanda Manyama akionyesha bunduki hiyo

Tue, 7 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mtu mmoja anayeaminika kuwa ni raia wa Burundi ameuawa na wananchi kwa tuhuma za kujaribu kufanya tukio la uporaji kwa kutumia bunduki ambapo pamoja na kifo hicho bunduki moja aina ya AKA 47 imekamatwa.

Kamanda wa polisi mkoa Kigoma, James Manyama akitoa taarifa kwa waandishi wa habari mjini Kigoma leo amesema kuwa mtu huyo ambaye jina lake halijafahamika hadi sasa alitaka kutenda tukio hilo jana jioni katika kijiji cha Kibuye wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma.

Kamanda Manyama alisema kuwa awali kabla ya kutekeleza azima yake hiyo marehemu akiwa amejificha kwenye kichaka alikutana na mwananchi mmoja wa kijiji hicho aliyefahamika kwa jina la Yapemacho Kasiano ambaye alimuhoji marehemu sababu ya kujificha kichakani ambapo Marehemu alijibu kuwa alikuwa anatafuta njia ya kwenda Burundi.

Alieleza kuwa wakiwa kwenye majadiliano hayo ndipo Marehemu alitoa bunduki aliyokuwa ameficha kwenye koti lake na kumshambulia nayo mwananchi huyo ambapo hata hivyo risasi ilimkosa Mwananchi huyo na ndipo akamrukia Marehemu na kuanza kupigana akitaka kumnyang’anya Bunduki huku akipiga kelele.

Kufuatia kelele hizo wananchi walijitokeza kwa wingi na kuanza kumshambulia Marehemu kwa silaha mbalimbali za jadi ikiwemo mikuki na mapanga ambapo alifariki dunia akiwa njiani kupelekwa hospitali baada ya kuvuja damu nyingi.

Katika tukio hilo Kamanda Manyama alisema kuwa pamoja na kifo cha marehemu pia polisi walikamata bunduki moja aina ya AK 47, risasi nne na ganda moja la risasi ambayo imetumika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live