Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mpiga picha wa Sabaya atoa ushahidi kesi ya kina Mbowe

Shahdipicc Mpiga picha wa Sabaya atoa ushahidi kesi ya kina Mbowe

Wed, 27 Oct 2021 Chanzo: mwananchidigital

Shahidi wa pili upande wa Jamhuri katika kesi ya ugaidi inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu, Justine Eliya Kaaya ameanza kutoa ushahidi.

Kaaya ambaye alikuwa mpiga picha wa aliyekuwa Mkuu wa Wilaya Hai, Lengai Ole Sabaya ametoa ushahidi huo leo Jumatano Oktoba 21, 2021 katika Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu.

Ifuatayo ni ushahidi wa mpiga picha Kaaya

Shahidi: Naitwa Justine Eliya Kaaya, nafanya kazi za kilimo cha mbogamboga yaani nyanya, vitunguu na viazi mbatata

Chavula: Taratibu jaji asikie

Hebu rejea nafaka unamaanisha nini

Shahidi: Mahindi na maharage nazifanyia Wilaya Arumeru Arusha

2017 nilikuwa naishi Wilaya ya Longido mkoa wa Arusha. Nilikuwa nashughulika na upigaji picha na pia kilimo Arumeru

Wakati huo nilikuwa nimelima karoti na mahindi. Wateja wangu walikuwa ni kutoka masokoni.

Upigaji picha nilikuwa napiga picha za mnato. Nilikuwa nawapigia viongozi wa Serikali na wa kisiasa

Viongozi hao walikuwa Dk Steven Lemomo Kiruswa mbunge wa Longido. Mrisho Mashaka Gambo aliyokuwa RC Arusha, Gabriel Nyagaro aliyokuwa DC Arusha mjini na wengine

Serikalini alikuwemo Lengai Ole Sabaya

Sabaya mara kwanza nilikutna naye 2017 katika uchaguzi mdogo Longido. Wakati huo alikuwa Diwani kata ya Sambasha, Arumeru na alivutiwa upigaji wangu wa picha

Sabaya alinitaka nikamsaidie kazi hiyo na shughuli nyingine mbalimbali ndani ya kata yake.

Nilimkubalia kwa sababu ilikuwa Ni fursa kwangu

Nilihama Longido kwenda Arusha, nyumbani kwa Sabaya Kibanda Maziwa, Sakina.

Nilikuwa nikiishi na Sabaya na mkewe

Nilifanyakazi naye hadi 2018 Julai alipoteuliwa kuwa DC Hai, nilienda kuishi naye katika makazi ya DC Hai Kilimanjaro.

Hapo nilikuwa msaidizi wake katika shughuli ndogondogo Kama kumpelekea nguo zake drycleaner, chai na chakula ofisini kila siku.

Hapo niliishi na Sabaya na mkewe.

Niliishi hapo tangu Julai 2018 Hadi mwezi wa 10,2018. Niliamua kurudi Longido kuendelea na majukumu yangu mengine, sababu niliacha mchumba na nilitaka nikusimamie shughuli zangu za kilimo.

Mwezi Novemba 2018 siku moja jioni nikiwa nyumbani nilipigwa simu kwa namba yangu ya airtel 0693006700 na namba ya Airtel 0784779944 na mtu aliyejitambulisha Kama Freeman Mbowe. Kwanza nilistuka. Kabla sikuwahi kuqasiliana naye.

Aliponipigia aliniuliza hujambo nikamwambia sijambo akasema nina shida ya kukuona ni muhimu Sana. Nilimuuliza aliko akanijibu yuko Arusha. Nikamwambia niko Longido na nina changamoto ya usafiri.

Aliniambia chukua gari Noah nitakuja kulipa gharama baada ya wewe kufika Arusha

Lakini kwa sababu ya Ile hofu nilimwambia sitakuja kwanza ni kiongozi mkubwa simfahamu na sina ukaribu wowote na yeye.

Aliniambia subiri nakupigia akakata simu.

Baada ya muda alinipigia tena akaniambia niko njiani nakufuata Longido

Kwa sababu alishaniambia yuko njiani anakuja nilishindwa kumzuia nikasema acha nimsubiri nisikie anachotaka kuniambia

Baada ya dakika 40 alinipigia tena simu akaniambia njoo hapa uwanja wa mpira Longido.

Nilimuita bodaboda anipeleke pale. Nilikuta gari liko pale linanguruma

Muda huo ilikuwa saa tatu usiku

Nikimpigia simu kwenye namba ileile ya 0784779944, akaniambia sogea kwenye gari. Nikasogea akashusha kioo cha dirisha akaniambia ingia kwenye gari chief usiwe na wasiwasi. Nikamruhusu yule boda akaondoka nami nikafungua gari mlango wa nyuma nikaingia.

Alikuwemo yeye na upande wa dereva alikuwepo mwanamke.

Aliniambia kwamba Lengai anasumbua Sana pale Hai na mimi Ni mtu wake wa karibu. Akawa anataka nimpe taarifa ya shughuli anazofanya na watu ambao yuko nao pale Hai. Nikamwambia haitawezekana sababu mimi sipo tena na Sabaya.

Aliambia yeye ni kiongozi wa Chama Kikuu cha Upinzani kwenye nchi hii, hivyo atafanya namna yoyote atakayoweza nirudi kwa Sabaya niendelee na kazi. Nilimwambia haitawezekana sababu nimechagua kufanya kazi zangu binafsi.

Aliniambia samahani kwa kukusumbua na alinipa Sh300,000

Nilimuuliza ni za nini akaniambia ni za usumbufu. Tutawasiliana. Tuliagana na aliondoka

Nilishuka kwenye gari nikampigia Lengai simu nimpe taarifa lakini hakupokea simu.

Niliendelea kusimama pale uwanjani na baadaye nilimpigia mbunge wa Longido Dk Steven Kiruswa kumweleza habari hizo. Nilimuita boda boda nikarudi nyumbani.

Mwanzoni mwa mwaka 2020, Januari alinipigia tena simu kwa mtandao wa WhatsApp kwa namba ileile baada ya salamu aliniambia tumepotezana Sana Chief, aliniambia anataka tuonane, nimfuate Moshi, wakati huo mimi nilikuwa Arusha. Nilimwambia niko shambani kumwagilia nikishamaliza nitakuja.

Baada ya shughuli zangu nilipanda Coster nikampigia simu kumpa taarifa kwamba naenda.

Baada ya kumpa taarifa aliniambia nishuke Machame Road, Wilaya ya Moshi mkoa wa Kilimanjaro.

Baada ya kufika nilishuka kwenye gari na kumpigia siku namba yake ileile ya Airtel. Aliniambia nisubiri hapo anakuja.

Baada ya muda akanipigia simu akaniambia nimefika umekaa upande upi nikamwambia nimekaa upande wa kushoto akaniambia njoo upande wa kulia. Kuna njia ya Machame na nyingine Arusha.

Ilikuwa gari V8 nyeusi yenye mlingoti na bendera ya Bunge yenye plate number KUB.

Ilisimama karibu yangu ikashusha kioo cha upande wa abiria. Nikamuona mwenyekiti Fewman Mbowe akaniambia panda. Alishuka mtu kutoka kwenye seat ya abiria nyuma akaniambia pita.

Tuliendelea kuzungumza ile gari ilichukua uelekeo wa Machame, baada ya dakika 8 iliingia mahali ni Hotel ya Aishi.

Shahidi huyo anaendelea kutoa ushahidi huo mahakamani hapo

Kulikuwa na dereva na huyo mlinzi wake aliyenipisha nikaingia kwenye gari. Nilikuwa sifahamiani nao.

Aliyenipisha nilijua ni mlinzi wake baada ya kunitambulisha kuwa Ni mlinzi wake Kanda ya Kaskazini na pia ni Diwani wa kata ya Kibororoni

Ile hotel nilitambua kwa sababu niliona kibao kilichoandikwa Aishi Hotel.

Baada ya kushuka kwenye gari mimi, yeye Mbowe na yule mlinzi wake, tulienda kuketi upande wa mgahawa, hoteli ya Aishi, akaniambia tutazungumza kwa muda mfupi kwa sababu ana mikutano ndani ya Jimbo.

Aliniambia niagize kinywaji au chakula.

Muda huo ilikuwa mchana saa 7 na simu ya kunitaka tukutane alinipigia saa 2:30 asubuhi.

Safari ya kuelekea Moshi( toka Arusha) nikiianza saa 5 kasoro.

Niliqnzia sehemu panaitwa Kilala ndani ya Wilaya ya Arumeru.

Kwanza Mbowe aliuliza kuna mipango gani juu ya hii mikutano ninayoifanya jimboni nikamwambia sijui chochote kinachoendelea. Aliniambia nimtajie majina ya wasaidizi wa Sabaya anaotembea nao, nilimwambia Sina taarifa yoyote ya kumweleza. Nilimtajia Yale majina na yule Diwani akawa anayaandika kwenye karatasi, majina ya Japhet Lwendela, Vedastus Sigula, Mtoto wa Mkulima, Sylvester a

Nyegu, Binti wa Kichaha Walimu Doreen, Watson Malimungu.

Akitaka na namba zao za simu pia. Nilitoka namba kwenye simu nimawqtajia wakaziandika, aksema atashughulika nao tutawasiliana Mimi na yeye baadaye.

Baada ya mazungumzo Freeman Mbowe aliniaga kwamba anakwenda kwenye mikutano na kwamba baadaye atanitumia chochote kwenye simu yaani nauli. Alitimiza Ile ahadi lakini hakunitafuta baada ya pale. Baada ya pale nikirudi Arusha.

Mwezi wa 7 2020, Siikumbuki tarehe, alinipigia kwa namba yake ya Airtel kwa njia ya mtandao wa WhatsApp namba ya 0784779944, aliniambia niko njiani natoka Dar naomba jioni tuonae nina jambo la muhimu kuzungumza na wewe uje Moshi. Wakati huo nilikuwa shambani kwangu na ilikuwa mchana saa 8.

Niliendelea kufanya shughuli zangu ilipofika saa 11 jioni nilianza safari ya kwenda Moshi, nilipanda Basi la Kiumbocharo liliokuwa likitoka Singida. Aliniambia kuanzia saa 1 atakuwa amefika Moshi. Nilishuka Moshi stendi saa 1:30 usiku.

Nilimpigia Freeman Mbowe simu namba yake ileile nikamwambia nimefika. Aliniambia nichukue pikipiki nimfuate Kizo hotel mjini Moshi.

Nilichukua bodaboda nikamwambia nipeleke Kizi hotel nikifika nikampigia Freeman Mbowe simu 0784779944 nikamwambia nimefika. Aliniambia namtuma msaidizi wangu akufuate. Baada ya muda alikuja dereva wake ambaye namkumbuka kwa jina moja la Willy, sababu tulipokutana mara ya kwanza Machame ndiye alikuwa anamwendesha.

Tulienda nyuma ya hotel ambako kuna swimming. (Willy) aliniambia Mheshimiwa yuko kwenye kikao, hivyo tukae hapa tumsubiri amalizie kikao.

Japo tulikuwa na mlinzi wake ambaye alikuwa baunsa kidogo, ambaye Willy aliniambia kuwa nisiwe na wasiwasi

Tulikula yule mlinzi wake aliekea alikokuwa Mbowe baada ya muda mfupi alirudi akasema tunaondoka.

Aliniambia (Freeman Mbowe) pole Sana kwa kukuweka, yule mlinzi wake alinifungulia mlango wa gari na yeye mwenyekiti aliingia na nyuma aliingia aliyokuwa mbunge wa viti Maalum Joyce Mukya nikakaa katikati na upande wa nyuma wa The. Mbowe akakaa mlinzi wake.

Baada ya pale kutoka Kizo hotel gari ilielekea uelekeo wa Arusha mpaka Aishi Hotel Machame.

Baada ya kushuka kwenye gari akimwambia yule mbunge atangulie ndani sisi tuna kikao kifupi.

Tulikaa upande wa mgahawa, Freeman Mbowe, mlinzi wake, dereva alipotaka kujumuika akimwambia hiki kikao ni cha watu watatu wewe kaa pembeni hakikuhusu.

Alinitambulusha akiniambia yule ni mlinzi wake na msiri wake anaitwa Halfan Bwire hivyo niwe huru kujumuika naye.

Huyo mlinzi tulikuwa tumekaa naye mkono wake wa kushoto.

Aliniambia nimtajie tena majina ya wale wote watu wa Sabaya na namba zao za simu na kazi wanazozifanya kw Sabaya. Kabla sinaanza kumtaja alimwambia mlinzi wake yule Halfani Bwire a hukue kalamu na karatasi ili aandike. Baada ya kurudi aliniambia nimwandikie. Hivyo nilianza kuandika majina na namba za simu.

Wale walikuwa Ni marafiki zake na Sabaya ambao nilikuwa nawafahamu na namba zao za simu nilikuwa nazo kwenye simu maana tulikuwa tunafahamiana.

Majina aliyoandika Ni Yale ya mwanzo nyongeza ni Enock Kirigiti.

Baadaye alinitaka nimtajie mahali Sabaya anapenda jutembelea, nilimtajia.

Anataja clubs mbalimbali pamoja na hotel mbalimbali ambazo Sabaya alkuwa anapenda kulala.

Baada ya kutoa Taatifa hizo nikimuuliza mwenyekiti hizi simj unataka za Nini? Akaniambia hilo niachie mimi kazi yako hapa imeisha.

Baada ya pale aliniambia nimkabidhi Halfani Bwire yale majina, Halfani Bwire akasema huyu Sabaya ni mtu mdogo sana nitamchezesha

Baada ya pale mwenyekiti aliniambia kazi imeanza rasmi kuanzia sasa hivi nitakuwa nakulipa mshahara.

Muda huo ilikuwa ni saa 4 usiku.

Baada ya pale alisema utapewa chumba ulale hapa utaondoka asubuhi . Sababu sikuweza kupata usafiri kwenda Arusha ikibidi nilale pale. Asubuhi Ile alinitumia Sh200,000 0754916666 kutoka namba yake ya Airtel, airtelmoney 0784779944.

Kulipokucha nilirudi Arusha saa 12 Asubuhi kuendelea na shughuli zangu za shambani

Hatukuwa ikianza tena kwa sababu tarehe 25 Agosti, 2020 nilikamatwa na Jeshi la Polisi.

Nilikamatwa Makumira wilaya ya Arumeru nikiwa naenda benki ya CRDB kupeleka hela.

Nilkuwa napeleka Fedha baada ya kuuza mazao ya shambani karoti ambayo nilikuwa ninewauzia watu wa Mount Meru. Nilikuwa na Sh1,117,000 Dola 1,100 za Marekani naEuro 240

Niipokamatwa nilipelekwa kituo iikuu cha Arusha na baada ya saa moja nikienda kupekuliwa nyumbani kwangu kksha nilisafirishwa kuletwa Dar.

Zile pasa zangu zilichukuliwa na Askari wakasema ni noti bandia.

Waliniambia nina tuhuma za kula njama za kufanya vitendo vya ugaidi.

Nilipofikishwa Dar nilipelekwa kituo kikuu cha Polisi Dar nikafanyiwa mahojiano na afande Mahita. Niliwekwa lockup hadi nilipokuja kufikishwa mahakamani Kisutu na kusomewa mashtaka mbalimbali ikiwemo, kushiriki vikao vya ugaidi, kulq njama za ugaidi, kesi ya utakatishaji wa fedha, nikaunganishwa na wenzangu ambao tayari walikuwa gerezani watatu,Halfan Bwire, Mohamed Ling'wenya na Adamu Kasekwa.

Halfani Bwire kabla ya kuunganisha naye nilikugana naye Kizi Hotel na Aishi Hotel akiwa na Mheshimiwa Freeman Mbowe.

Mohamed Ling'wenya nilikuwa simfahamu ndio ilikuwa mara ya kwanza na Adamu Kasekwa nilikuwa simfahamu pia.

Baada ya kuunganishwa kwenye kesi hiyo Kisutu nilipelekwa gereza la Ukonga. Hapo nilikuwa na Halfan Bwire, baadaye akaletwa Khalid Athuman na baadaye akaletwa Mohamed Ling'wenya kutoka Segerea.

Nimekuwa kwenye kesi Ile kwa miezi 11.

Tarehe 26 Julai 202@ jioni aliletwa Mheshimiwa Mbowe gerezani Ukonga akanikuta na Halfan Bwire akasema poleni sana nimekuja kuwatoa.

Tulilala na ilipofika asubuhi watu wa Magereza walikuja wakasema jiande kupelekwa mahakamani. kwsho yake tarehw 27 tulipelekwa mahamani watatu Mimi mshtakiwa wa nne, Khalid Athuman I was sita na Gabriel Mhina mshtakiwa wa sita. Wakili wa Serikali alisema baada ya upelelezi kukamilisha hakuna ushahidi tukafutiwa mashtaka.

Zile Fedha zangu nikienda Mahakama Kisutu nikaelekwa Central nikakuta Mkavuzi Msaidizi Swila akaniandika maelezo uhusiano wangu na nilivyofahamiana na Mhe. Mbowe, baada ya muda nilipewa vitu vyangu vyote.

Mbowe, Halfani Bwire, Mohamed Ling'wenya na Adamu Kasekwa kwa Sasa wako hapa mahakamani.

Wakili wa Serikali Chavula anamtaka shahidi awaoneshe kwa majina na Shahidi anawasogelea na kuwataja kwa majina huku akiwasonda kwa kidole akianza na Halfan Bwire, Adamu Kasekwa, Mohamed Ling'wenya na Mbowe. Kisha anarejea kizimbani.

Wakili: Mheshimiwa kwa sasa ni hayo.

Mawakili wa pande zote Sasa wanajadiliana

Kibatala: Tunapendekezo kwa afya za washtakiwa tu-break for thirty minutes.

Upande wa mashtaka: Hatuan pingamizi.

Jaji; Mniambie turudi muda gani.

Kibatala: Saa 8:25

Kesi imeahirishwa kwa muda hadi saa 8:25 ambapo mawakili wa Utetezi wataanza kumhoji shahidi.

Chanzo: mwananchidigital