Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mpagazi aliyefungwa maisha jela Moshi ana kesi nyingine ya kulawiti

31461 Kesi+pic TanzaniaWeb

Thu, 13 Dec 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Moshi. Mbeba mizigo ya watalii aliyehukumiwa kifungo cha maisha jela kwa kulawiti watoto watatu wa kiume, anakabiliwa na kesi nyingine ya ulawiti.

Mpagazi huyo, George Lesilwa (33) ambaye hutoa huduma Mlima Kilimanjaro, anadaiwa kutenda kosa hilo baada ya kuhama chumba alichokuwa akiishi awali eneo la Kiborlon Mnazi, Moshi mwaka 2017, baada ya kushitakiwa kwa kulawiti vijana hao watatu.

Baada ya kufikishwa kortini mwaka 2017 kwa tuhuma za kuwalawiti watoto hao watatu, mtuhumiwa huyo alihama na kupanga chumba eneo la Majengo.

Huko anatuhumiwa kumlawiti mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka 11 na hivyo kufunguliwa kesi mpya namba 262/2018 iliyopo mbele ya Hakimu Mkuu Mkazi Mfawidhi wa Moshi, Bernazitha Maziku.

Upande wa mashitaka katika kesi hiyo inayoendeshwa na Wakili Mwandamizi wa Serikali, Tamari Mndeme unadai mshitakiwa alitenda kosa hilo kati ya Aprili na Mei, 2018 akiwa Majengo.

Kesi hiyo imepangwa kuanza kusikilizwa rasmi kesho, wakati mshitakiwa huyo akiwa ameshahukumiwa kifungo cha maisha katika kesi nyingine ya kulawiti.

Juzi Hakimu Mkuu Mkazi, Pamela Mazengo alimpa Leswila kifungo cha maisha kwa kila kosa la kulawiti watoto hao watatu wa kiume.

Kwa mujibu wa ushahidi uliotolewa kortini, mshitakiwa alikuwa akiwalawiti watoto hao kwa nyakati tofauti Oktoba 2017, na kisha kuwapa Sh500 kila mmoja anapotimiza haja zake.

Mawakili wa Serikali, Ignas Mwinuka na Grace Kabu, walikuwa wameomba mahakama impe mshtakiwa adhabu kali kwa vile vitendo hivyo vinaendelea kuongezeka nchini.



Chanzo: mwananchi.co.tz