Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Morani wa Kimasai adaiwa kujinyonga Kiteto

Morani Ajinyonga Eeeeh Bwana Weeee Ni Balaaa.png Morani wa Kimasai adaiwa kujinyonga Kiteto

Mon, 23 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kijana wa Kimasai rika la Morani, aliyejulikana kwa jina Sabaya Isaskar (31) mkazi wa Njaniodo, wilayani Kiteto mkoani Manyara amedaiwa kujinyonga hadi kufa kwa kutumia kamba ya manila.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Partimbo, Kimirei Mesiaya amethibitisha kutokea kwa kifo hicho leo Jumatatu Oktoba 23, 2023 akisema marehemu alikutwa porini juu ya mti ananing’inia na wasamaria wema waliokuwa wakipita kilometa 3 kutoka nyumbani kwake baada ya kujinyonga.

"Nilipokea taarifa ya mtu kujingonga porini na baadaye nikafuatilia na kubaini kifo hicho ambacho kwa kweli kinasikitisha sana… kwani aliyepoteza maisha hakuwa mgonjwa bali ameamua kuchukua maamuzi magumu ya kujiua," amesema Mesiaya.

Amesema watu walipata mshtuko mkubwa kusikia mtu kujinyonga na leo tunashiriki mazishi yake.

Ameongeza kuwa hali haikuwa nzuri awali kila mmoja hapa alionekana mwenye masikitiko na huzuni.

"Mmasai kujinyonga ni nadra sana kusikia kama hivi leo…Tumezoea kusikia makabila mengine kuwa mtu amejinyonga lakini kwa Mmasai hasa kijana siyo hali ya kawaida," amesema Lasingoo Mollel ambaye ni mkazi wa Lairupa.

Hata hivyo, tabia iliyojengeka kwa baadhi ya watu kutotoa taarifa ya kifo Polisi anapokutana na matukio hayo kukihofia kusaidia jeshi hilo kupata taarifa, hali hiyo imeendelea kujitokeza baada ya taarifa kuchelewa kutolewa kuhusu kifo cha kijana huyo.

"Nilitoa taarifa lakini nilikuwa ninaogopa kwa sababu huwa nasikia watu wanasema ukitoa taarifa nitafungwa…Polisi huwa wanauliza huyu mtu mpaka umemuona mlikuwa mnafanya nini, hata hivyo nikaamua kumpigia mwenyekiti wa kijiji kumwambia kuna tukio kule porini," amesema mkazi wa eneo hilo Chekuu Ngelelili.

Baadhi viongozi wa mila wa jamii ya kufugaji Maasai wamesema tukio hilo halikuzoeleka kwa jamii hiyo hivyo watakaa pamoja kutafuta undani wa tukio hiko.

"Tangu nimezaliwa nina miaka 78 sijawahi kuona tukio kama hili kwa Mmasai kujinyonga lakini kwa mwaka huu nimeona kwa watu wa makabila makabila mengine…ni mshangao mkubwa kwa Wamasai nini kimesababisha huyu kijana afariki dunia?” amehoji Laisingoo Parmet.

Kaka wa marehemu, Meshack Saskari ameeleza kuhusu kifo hicho akisema kimekuwa cha ghafla na kwamba hakuwa anaumwa.

"Kifo hiki kinasikitisha kwa sababu alikuwa hajaugua alikuwa na familia yake ya mke na watoto wawili vile vile ana ngombe wake zaidi ya 20 mashamba na chakula cha kusikitisha alikwenda porini mwenyewe na kujinyonga," amesema Meshack.

Mchungaji Ruben Kitimu wa Kanisa la KKKT Kibaya, amesema maisha ni zawadi kutoka kwa Mungu hivyo hakuna sababu ya mtu kukatisha maisha yao.

"Maisha ni zawadi aliyotupa Mungu kwa hiyo tunapaswa kulinda maisha yetu ambayo Mungu ametupa kama zawadi," ame

Chanzo: www.tanzaniaweb.live