Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Monica ajiua kwa kamba ya katani

Mwakyoma.png Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Manyara, Kamishna Msaidizi (ACP) Merrisone Mwakyoma

Fri, 15 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkazi wa Kijiji cha Riroda wilayani Babati mkoani Manyara Monica Manyara, (65), amefariki dunia baada ya kujinyonga kwa kutumia kamba ya katani Oktoba 13, 2021 majira ya saa moja asubuhi ambapo chanzo cha kifo hicho bado hakijajulikana.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Manyara, Kamishna Msaidizi (ACP) Merrisone Mwakyoma, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo, ambapo amesema inadaiwa kuwa kabla ya kifo hicho marehemu walishawahi kujaribu kijinyonga kwa zaidi ya mara tatu kwa siku tofauti bila mafanikio.

Amesema kabla ya kifo chake Monica alitoweka nyumbani kwake mnamo Oktoba 8 mwaka huu na kutokomea kusikojulikana.

"Ndugu zake walimtafuta kwa siku zote hizo hadi wakamkuta kajinyonga mlimani kwa kamba siku hiyo ya tukio," amesema kamanda Mwakyoma.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live