Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mmoja auawa mkoani Kilimanjaro

Mmoja Auwawapic Auawa

Wed, 15 Sep 2021 Chanzo: Mwananchi

Denis Chuwa (21) mkazi wa kitongoji cha Manjaro kata ya Uru Mashariki wilayani Moshi ameuawa na watu wasiojulikana na mwili wake kutelekezwa pembezoni mwa barabara ya kuelekea Uru Shimbwe.

Akizungumza leo Jumatano Septemba 15, 2021 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa amesema tukio hilo limetokea Jumanne Septemba 14, 2021 na kwamba mwili huo ulikutwa umekatwa na kitu chenye ncha kali.

“Msako mkali unaendelea kuwatafuta waliotenda mauaji ya kijana huyu anayedaiwa kuwa alikuwa na tatizo la akili, inaonekana amekatwa na kitu chenye ncha kali shingoni . mwili wake umehifadhiwa hospitali ya KCMC,” amesema.

Chanzo: Mwananchi